Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Maneno hayo ameyazungumza leo 26/06/2026 Wilaya ya Magu alipomuwakilisha Mkuu wa Mkoa Wa Mwanza, Said Mtanda Kwenye kilele hicho cha Maadhimisho ya kuzuia na kupambana na Dawa za kulevya Kanda ya ziwa.
Katika Mazungumzo yake na Wandishi wa Habari, Kaimu Kamishina wa Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Kanda ya Ziwa, Wamba Msafiri amesema "Sisi Mamlaka tunajipanga kila siku kuzuia Dawa za kulevya kadili wauzaji na wazalishaji wanavyobadili mbinu za uuzaji kwani Wahalifu hawa hubuni mbinu mpya za uuzaji wa Dawa za kulevya na Sisi kama mamlaka, tunazidi kuongeza mbinu za kukabiliana nao."
Upande wa Esther Morris, Mkurugenzi wa Taasisi ya Naweza Tena ya Mwanza amesema wapo watu ambao wanatumia Wanafunzi wa Shule za Msingi kusambaza Dawa za kulevya, hivyo kuwa ngumu kuwatambua kwa urahisi, maana wengi wao hubeba bidhaa hiyo kwenye begi za Daftari, ni ngumu kuwakagua, hivyo Wazazi tunapaswa kuwa Makini na watoto pamoja na kuwakagua mara kwa mara kila waendapo na kutoka shule."