DC Ludigija: Atoa wito Wananchi kushirikiana na Serikali kupambana na Dawa za kulevya Nchini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Your browser is not able to display this video.
Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Mwilabuzu Ludigija amewataka Wananchi kushirikiana na Serikali kwenye Mpango wa kuzuia na kupambana na Dawa za kulevya Nchini kwani jukumu hilo sio la Serikali pekee.

Maneno hayo ameyazungumza leo 26/06/2026 Wilaya ya Magu alipomuwakilisha Mkuu wa Mkoa Wa Mwanza, Said Mtanda Kwenye kilele hicho cha Maadhimisho ya kuzuia na kupambana na Dawa za kulevya Kanda ya ziwa.

Katika Mazungumzo yake na Wandishi wa Habari, Kaimu Kamishina wa Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Kanda ya Ziwa, Wamba Msafiri amesema "Sisi Mamlaka tunajipanga kila siku kuzuia Dawa za kulevya kadili wauzaji na wazalishaji wanavyobadili mbinu za uuzaji kwani Wahalifu hawa hubuni mbinu mpya za uuzaji wa Dawa za kulevya na Sisi kama mamlaka, tunazidi kuongeza mbinu za kukabiliana nao."

Upande wa Esther Morris, Mkurugenzi wa Taasisi ya Naweza Tena ya Mwanza amesema wapo watu ambao wanatumia Wanafunzi wa Shule za Msingi kusambaza Dawa za kulevya, hivyo kuwa ngumu kuwatambua kwa urahisi, maana wengi wao hubeba bidhaa hiyo kwenye begi za Daftari, ni ngumu kuwakagua, hivyo Wazazi tunapaswa kuwa Makini na watoto pamoja na kuwakagua mara kwa mara kila waendapo na kutoka shule."
 
Tunaishi mara moja tukiondoka haturudi, mwenye connection ya kazi hii tafadhali tuwasiliane
 
Dawa za kulevya ziko kila mahali, ni moja ya biashara kubwa mno.... ipo toka enzi na enzi na ni world wide........

Wanawapotezea wale mapapa wanaodili nazo ama kwa favor/kuhongwa, alafu wanadili na vile vidagaa vinavyosuplly makapi !!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…