Tatizo mnasoma kamstari kamoja ka sheria, halafu mnajiona tayari mnajua sheria.
Rais hana mamlaka ya kuhamisha watu. Mamlaka ya Rais ni kubadilisha matumizi ya ardhi tu. Na katika kubadilisha matumizi hayo ya ardhi, sharti kuu ni lazima mabadiliko hayo yawe kwa manufaa ya umma. Hivyo kwenye hili ni lazima mabadiliko hayo ya matumizi ya ardhi yathibitike moja kwa moja kuwa kuna manufaa makubwa ya umma, na uwepo wa masasai huko Ngotongoro ni hasara kwa umma. Lazima manufaa hayo yathibitike ni kwaajili ya umma, na siyo mwarabu.
Rais akishabadilisha matumizi ya ardhi ardhi, kinachofuata ni relocation plan ambayo inatakiwa izingatie mwongozo wa World Bank. Mwongozo huo unataka usimpeleke mbali uliyemhamisha kiasi cha kumfanya aliyehamishwa kukutana na mazingira tofauti kabisa ya tamaduni na shughuli zake za kiuchumi alizozizoea. Kwa hali iliyopo huwezi kusema kuna hasara za moja kwa moja za wamasai kuendelea kuwepo Ngorongoro. Na huwezi kusema kuwa uhamishaji wa wamasai ili kumridhisha mwarabu aliyepewa rasilimali za nchi kwa deals chafu, kuna manufaa ya moja kwa moja kwa nchi. Na hata kama kuna manufaa kwa umma, huwezi kusema kuwahamisha wamasai toka Manyara mpaka Tanga watakutana na mazingira yanayofanana kitamaduni na kishughuli za kiuchumi.