DC Magoti: Tuchore mstari ili kumsaidia Rais wetu - sema enough is enough

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
12,213
Reaction score
28,916
MKUU WA WILAYA YA KISARAWE

KISARAWE – PWANI

YAH: TAARIFA NA OMBI LA KUPATIWA MSAADA KUHUSU KERO YA KELELE ZA MUZIKI KUTOKA KWA BAR ILIYO KATIKATI YA MAKAZI

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya,

Hii ni mara ya pili nakuandikia hapa jamiiforums!

Ninakuandikia barua hii kwa heshima, na kwa mara ya pili, kwa kuwa ombi langu la awali halikupata ufumbuzi wa tatizo nililolieleza. Naomba ofisi yako ilichukulie suala hili kwa uzito na itoe msaada wa Serikali kuhusu kero kubwa tunayokumbana nayo mimi, familia yangu pamoja na majirani zangu tunaoishi katika eneo la Kiluvya Madukani, Makurunge, Kisarawe – Pwani, kwa Bibi Kivuzi.

Kero hii inamhusu mtu anayeitwa Massawe, ambaye ameanzisha baa katikati ya eneo la makazi ya wananchi. Tangu kuanzishwa kwa biashara hiyo, amekuwa akipiga muziki kwa sauti kubwa mara kwa mara, hususan nyakati za usiku.

Hali hii imekuwa ikituletea usumbufu mkubwa sisi wakazi wa eneo hilo. Muziki huo wenye sauti kubwa unavuruga utulivu wa familia zetu, unatunyima usingizi wa kutosha na kufanya maisha ya kawaida ya kifamilia kuwa magumu. Aidha, sauti na mtikisiko unaotokana na muziki huo hufika moja kwa moja katika nyumba za majirani, hivyo kutufanya tushindwe kupata mazingira tulivu ya kupumzika wakati wa usiku.

Tatizo kubwa zaidi ni kwamba shughuli hiyo imeanzishwa katikati ya makazi ya watu, hivyo kelele hizo zinawaathiri moja kwa moja wananchi wanaoishi jirani na eneo hilo. Tunaelewa kuwa mhusika ana haki ya kufanya biashara kwa mujibu wa sheria, lakini tunaamini pia kuwa haki hiyo inapaswa kutekelezwa kwa kuzingatia haki na ustawi wa majirani, pamoja na sheria na taratibu zinazohusu kelele na uendeshaji wa biashara katika maeneo ya makazi.

Hii ni mara ya pili nakuandikia kukuomba uje utusaidie uone kwa macho yako mwenye na kusikiliza waathiriwa maana wakati anajenga hii bar alitukuta sisi tukiishi hapa na wengine majirani zangu wapo mbele kabisa sijui wanaishije maana mimi nipo nyumba 4 kutoka kayika ukuta wa bar na siwezi hata kulala.

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya, tumejaribu kuvumilia hali hii na tumewahi kuwasilisha malalamiko kuhusu tatizo hili, lakini hadi sasa halijapata ufumbuzi wa kudumu. Kero hii imeendelea na sasa imekuwa kubwa kwa familia na majirani. Tunaomba Serikali, kupitia ofisi yako, ifanye uchunguzi na ukaguzi wa eneo hilo, pamoja na kuangalia uhalali wa uendeshaji wa baa hiyo katika eneo la makazi na hatua zinazoweza kuchukuliwa kudhibiti kelele zinazotusumbua.

Tunaomba pia mamlaka husika zifanye vipimo au tathmini ya kiwango cha kelele kinachotokana na muziki huo, hasa nyakati za usiku, na kuhakikisha kuwa shughuli hiyo haikiuki taratibu za mazingira, afya, usalama na utulivu wa wakazi wa eneo hilo Kwa kuwa wakati mwingine mziki unafunguliwa kuanzia saa 6 usiku na kuweka maneno ya vitisho kwa majirani ana jeuli sana huyu mtu

Kwa heshima kubwa, tunaomba Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya alichukulie suala hili kwa uzito, atoe maelekezo kwa mamlaka husika na kuhakikisha kuwa hatua stahiki zinachukuliwa ili tatizo hili lipate ufumbuzi. Tunaamini kuwa Serikali ipo kwa ajili ya kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wake.

kuna jirani yetu ametegewa spika kubwa (pichani) karibu kabisa na mlango wake kama sisi wa mita mia hatulali je huyo na wanaopakana kabisa na hiyo bar na tuko na waginjwa
Screenshot_20261006_145535_Instagram Lite.jpg

Lengo letu si kumzuia mtu kufanya biashara yake, bali ni kulinda haki yetu ya kuishi katika mazingira yenye utulivu na amani, bila usumbufu wa kelele zinazotokana na shughuli za biashara zinazofanyika katikati ya makazi.

View attachment 3685310

USSR
Nenda NEMC chap, huyo Mkuu wa Wilaya atakuchelewesha na huenda ana hisa!
 
hilo tatizo la kelele ni kazi ya mwenyekiti wa serikali za mitaa, ana uwezo wote wa kisheria kutatua ikiwa ni pamoja na kuifunga bar kwa kuamrisha polisi, yote anaweza kuayafanya kisheria, sema watanzagiza hatuelewi umuhimu wa cheo cha mwenyekiti wa serikali za mitaa na wengi tunakipuuzia hata kwenye vikao hatuendi, vile vikao ni kwa ajili ya kujadili yanayoendelea kwenye makazi yenu kama viwanja vya michezo vya vijana, wenye nyumba kuziba njia kwa kujenga ukuta pasipo ruhusiwa, viwanja vya shule kujengwa mafremu, usalama wa raia mitaani mpaka hata kukarabati br. za mitaa nafikiri bado mwenyekiti ana uwezo wa kukodisha greda yote haya yako chini ya mwenyekiti wa serikali za mitaa ambaye anachaguliwa na wananchi ...
 
hilo tatizo la kelele ni kazi ya mwenyekiti wa serikali za mitaa, ana uwezo wote wa kisheria kutatua ikiwa ni pamoja na kuifunga bar kwa kuamrisha polisi, yote anawezekan sema watanzagiza hatuelewi umuhimu wa cheo cha mwenyekiti wa serikali za mitaa na wengi tunakipuuzia hata kwenye vikao hatuendi, vile vikao ni kwa ajili ya kujadili yanayoendelea kwenye makazi yenu kama viwanja vya michezo vya vijana, wenye nyumba kuziba njia kwa kujenga ukuta pasipo ruhusiwa mpaka hata kukarabati br. za mitaa nafikiri bado mwenyekiti ana uwezo wa kukodisha greda yote haya yako chini ya mwenyekiti wa serikali za mitaa ambaye anachaguliwa na wananchi ...

Tatizo walijipachika madarakani hiyo kelo sio mpaka mwananchi uende serikali ya mtaa serikali ya mtaa ilitakiwa kufanya majukumu yake bila
Kukumbushwa kwana si wanaskia hizo kelele
 
MKUU WA WILAYA YA KISARAWE

KISARAWE – PWANI

YAH: TAARIFA NA OMBI LA KUPATIWA MSAADA KUHUSU KERO YA KELELE ZA MUZIKI KUTOKA KWA BAR ILIYO KATIKATI YA MAKAZI

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya,

Hii ni mara ya pili nakuandikia hapa jamiiforums!

Ninakuandikia barua hii kwa heshima, na kwa mara ya pili, kwa kuwa ombi langu la awali halikupata ufumbuzi wa tatizo nililolieleza. Naomba ofisi yako ilichukulie suala hili kwa uzito na itoe msaada wa Serikali kuhusu kero kubwa tunayokumbana nayo mimi, familia yangu pamoja na majirani zangu tunaoishi katika eneo la Kiluvya Madukani, Makurunge, Kisarawe – Pwani, kwa Bibi Kivuzi.

Kero hii inamhusu mtu anayeitwa Massawe, ambaye ameanzisha baa katikati ya eneo la makazi ya wananchi. Tangu kuanzishwa kwa biashara hiyo, amekuwa akipiga muziki kwa sauti kubwa mara kwa mara, hususan nyakati za usiku.

Hali hii imekuwa ikituletea usumbufu mkubwa sisi wakazi wa eneo hilo. Muziki huo wenye sauti kubwa unavuruga utulivu wa familia zetu, unatunyima usingizi wa kutosha na kufanya maisha ya kawaida ya kifamilia kuwa magumu. Aidha, sauti na mtikisiko unaotokana na muziki huo hufika moja kwa moja katika nyumba za majirani, hivyo kutufanya tushindwe kupata mazingira tulivu ya kupumzika wakati wa usiku.

Tatizo kubwa zaidi ni kwamba shughuli hiyo imeanzishwa katikati ya makazi ya watu, hivyo kelele hizo zinawaathiri moja kwa moja wananchi wanaoishi jirani na eneo hilo. Tunaelewa kuwa mhusika ana haki ya kufanya biashara kwa mujibu wa sheria, lakini tunaamini pia kuwa haki hiyo inapaswa kutekelezwa kwa kuzingatia haki na ustawi wa majirani, pamoja na sheria na taratibu zinazohusu kelele na uendeshaji wa biashara katika maeneo ya makazi.

Hii ni mara ya pili nakuandikia kukuomba uje utusaidie uone kwa macho yako mwenye na kusikiliza waathiriwa maana wakati anajenga hii bar alitukuta sisi tukiishi hapa na wengine majirani zangu wapo mbele kabisa sijui wanaishije maana mimi nipo nyumba 4 kutoka kayika ukuta wa bar na siwezi hata kulala.

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya, tumejaribu kuvumilia hali hii na tumewahi kuwasilisha malalamiko kuhusu tatizo hili, lakini hadi sasa halijapata ufumbuzi wa kudumu. Kero hii imeendelea na sasa imekuwa kubwa kwa familia na majirani. Tunaomba Serikali, kupitia ofisi yako, ifanye uchunguzi na ukaguzi wa eneo hilo, pamoja na kuangalia uhalali wa uendeshaji wa baa hiyo katika eneo la makazi na hatua zinazoweza kuchukuliwa kudhibiti kelele zinazotusumbua.

Tunaomba pia mamlaka husika zifanye vipimo au tathmini ya kiwango cha kelele kinachotokana na muziki huo, hasa nyakati za usiku, na kuhakikisha kuwa shughuli hiyo haikiuki taratibu za mazingira, afya, usalama na utulivu wa wakazi wa eneo hilo Kwa kuwa wakati mwingine mziki unafunguliwa kuanzia saa 6 usiku na kuweka maneno ya vitisho kwa majirani ana jeuli sana huyu mtu

Lengo letu si kumzuia mtu kufanya biashara yake, bali ni kulinda haki yetu ya kuishi katika mazingira yenye utulivu na amani, bila usumbufu wa kelele zinazotokana na shughuli za biashara zinazofanyika katikati ya makazi.

Kwa heshima kubwa, tunaomba Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya alichukulie suala hili kwa uzito, atoe maelekezo kwa mamlaka husika na kuhakikisha kuwa hatua stahiki zinachukuliwa ili tatizo hili lipate ufumbuzi. Tunaamini kuwa Serikali ipo kwa ajili ya kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wake.

kuna jirani yetu ametegewa spika kubwa (pichani) karibu kabisa na mlango wake kama sisi wa mita mia hatulali je huyo na wanaopakana kabisa na hiyo bar na tuko na waginjwa
View attachment 3685310

USSR
Kwa ninavyomfahamu huyu DC lazima atachukua hatua siyo mtu wa kupenda kero labda awe anashea zake kwenye bar hiyo. Vinginevyo hii kero itamtia doa kubwa maana lazima awajibike kuwahakikishia usalama wananchi wake
 
kwa Bibi Kivuzi
Huu mtaa, hakukua na jina jingine?

Sema bar karibu na makazi ya watu zinazingua. Imagine watoto , wagonjwa, Wanafunzi kujisomea.

NEMC walitoa msimamo kuhusu makelele na wakaweka max decibels (dB) ila ishapita kama hivi.
 
Unamwandikia Mkuu wa Wilaya Ili afanye nini? Kwani yeye ni Polisi? Na, je huo mtaa hauna viongozi wa serikali ya mtaa?

Kumhusisha DC kwa ishu mdogo kama hii ni kuonesha kuwa mifumo ya kiserikali from the bottom ime - paralyze, haitendi kazi yake ipasavyo na ndio maana tunataka constitutional reforms Ili kuhuisha mifumo ya kiserikali ipate nguvu ya kutenda kazi tena!!

Nyie ndio ndio mnawafanya watu kama hawa maDC, RCs na mpaka mawaziri wajinga kama Patrobas Katambi wafanye majukumu yasiyowahusu kabisa na matokeo yake wanakosea na kuharibu..

Hilo ni jukumu/kazi ya Polisi pia. Sometimes hawahitaji hata kuletewa taarifa kwa sbb uhalifu mwingine Polisi wanaweza kuuona wazi kwa macho na kuzuia au kuchukua hatua bila hata kusubiri kuletewa taarifa na mtu au raia...

Hawa kazi yao ni kulinda usalama wa raia na ku-maintain LAWS and ORDERS katika jamii..

Ipo sheria inayosimamia taratibu za uendeshaji wa biashara au upigaji wa muziki. Huyo anayepiga muziki hovyo kiasi cha kuingilia haki za wengine kufurahia utulivu na amani katika nyumba zao, anavunja sheria hii..

Moja ya sharti lililo katika sheria hii kwa waendeshaji wa biashara ya muziki, ni kuwa, lazima ukumbi au eneo analopigia muziki wake kuwa na sound proof roof Ili kuzuia sauti kusambaa/kupaa na kusumbua wasiohusika..

Na tatizo hili la kupiga muziki hovyo (ambayo kwa kweli kwa wengine ni makelele na sio muziki) mitaani mchana kutwa, usiku lipo kila kila sehemu ya miji kuanzia miji midogo hadi mikubwa (cities)

Tatizo kubwa ni kuwa wengi wa Polisi wa Leo ni wajinga, hawazijui sheria wanazopaswa kuzi - maintain ili kuleta harmony katika jamii. Moja ya sheria ni hiyo inayoongoza ishu unsyoilalamikia..

Polisi kila siku wanafanya patrol. Wanashindwa nini kuziona/kusikia kelele hizo na kuchukua hatua? Au wanataka mpaka wakoromewe na DC au kiongozi fulani wa kisiasa/serikali ndo wachukue hatua kulinda watu toka kwa ukorofi wa watu fulani wachache..?

Peleka lalamiko au taarifa yako hii Polisi. Ni wazi watachukua hatua stahiki..
 
Imagine mtaa mzima hamlali

Kunab
Huyo massawe anafanya makusudi ili wakereke wahame atanue eneo lake la bar

wachague wamuuzie maeneo yao au wapige kiberiti bar yake!
Anasema anataka anunue mtaa wote kwa hiyo kelele zake ni lengo la watu tuhame anunue eneo lote

USSR
 
wakati mwingine mziki unafunguliwa kuanzia saa 6 usiku na kuweka maneno ya vitisho kwa majirani ana jeuli sana huyu mtu

Lengo letu si kumzuia mtu kufanya biashara yake, bali ni kulinda haki yetu ya kuishi katika mazingira yenye utulivu na amani,
Hapa mboni km unaogopa hivi?
 
Back
Top Bottom