Mkuu wa wilaya ya Makete mkoani Njombe Kissa Kasongwa ameagiza wakazi wa wilaya hiyo kuchukua tahadhari dhidi ya moto unaoteketeza misitu na kupoteza fedha nyingi kila mwaka hali inayopelekea kurudisha nyuma uchumi wa wanaMakete
DC Kissa ameeleza hayo wakati akizungumza na wakazi wa Bulongwa ambapo amesema wakazi wa wilaya hiyo hawana wivu wa mapenzi lakini wana wivu mkubwa kwenye misitu hali iliyopelekea kuchomeana miti na kusababisha hasara ya zaidi ya Bilioni 80 kwa miaka minne
“Huku hamna wivu wa mapenzi ila kuna wivu wa misitu sasa haya mambo hayafai,kwa miaka minne tu katika wilaya yetu ya Makete tumepata hasara ya kuunguliwa kwa moto na kupoteza zaidi ya Bilioni themanini ni hela nyingi sana na ninyi watu wa Makete mnaijua hela kwa hiyo sasa misitu hii lazima tuilinde kwa wivu mkubwa”amesema Kissa
Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Makete,Moses Ndiu ametaka tahadhari ziendelee kuchukuliwa kwa kiasi kikubwa kwa kuwa mwananchi anapopata hasara kwa kuunguliwa msitu inapelekea TFS na serikali kukosa mapato
Katika ziara hiyo DC Kissa ameambatana na kikundi cha vijana kutoka Kijiji cha Mago kwa ajili ya kutoa elimu kwa kuwa kijiji cha mfano katika wilaya hiyo kutokana na kufanikiwa kudhibiti moto ambapo wamefikisha miaka mitatu sasa bila kupata janga la moto