Mpepetaji
JF-Expert Member
- Mar 25, 2025
- 346
- 213
Mkuu wa wilaya ya Makete mkoani Njombe Kissa Gwakisa Kasongwa amezindua mradi wa maji uliopo chini ya wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) katika kijiji cha Ipepo wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 416.
Kasongwa amezindua mradi huo Machi 25, 2025 katika kijiji hicho na kueleza kufurahishwa na namna RUWASA Makete ilivyosimamia utekelezaji wa mradi huo na kueleza kuwa uwepo wake ni mwendelezo wa serikali ya awamu ya sita katika kuwaletea huduma wananchi wake hivyo amewasihi watunze miundombinu ya maji sambamba na kuonesha utayari katika ulipiaji wa ankara za maji pia kuliona zoezi la kufungiwa mita kuwa rafiki kwao.
Meneja wa wakala wa maji na usafi wa mazingira Vijijini RUWASA wilaya ya Makete Mhandisi Innocent Lyamuya amesema mradi huo baada ya kukamilika utawanufaisha wananchi wa kijiji cha Ipepo wapatao 1,015.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Makete Clement Ngajilo pamoja na Katibu wa chama hicho Daniel Mhanza wamesema kukamilika kwa mradi huo ni mwendelezo wa CCM katika kutekeleza ilani yake hivyo wamehimiza wananchi kuendelea kukiunga mkono chama hicho.
Diwani wa kata ya Ipepo Manase Nyaulawa pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji cha Ipepo Tadei Sanga wameishukuru serikali kwa kuendelea kupeleka miradi mbalimbali katika eneo hilo kwani hali hiyo imeendelea kuwanufaisha wananchi wake.