Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,307
- 25,932
Mkuu HAMY-D, ameweka video ya sakata la kuswekwa ndani kwa Watendaji wa Ardhi wa Kinondoni kwa amri ya Mkuu wa Wilaya hiyo,Mhe. Paul Makonda. Nimeitazama na kuisikiliza kwa makini sana video hiyo inayodaiwa ndiyo ufafanuzi wa kilichotokea. Swali hapa ni: Watendaji hao walitenda mmakosa ya aina gani? Katika utumishi wa umma kuna makosa ya aina mbili. Aina ya kwanza ni makosa ya jinai. Haya huweza kutendwa na watumishi wa umma na kupelekea wao kukamatwa nakushtakiwa na Jamhuri mahakamani.
Makosa ya jinai ni kama kuiba, kuua, kubaka,kulawiti, kunajisi, kujihusisha na kusafirisha na matumizi ya madawa ya kulevya na kadhalika. Aina ya pili ya makosa yanayoweza kutendwa na watumishi wa umma ni makosa ya kinidhamu. Makosa haya ni yale yanayohusika moja kwa moja na utendaji wa kazi wa mhusika. Makosa haya yanaainishwa chini ya Sheria za Kazi za Tanzania hasa Kanuni za Utendaji Bora, Tangazo la Serikali Nambari 64 la mwaka 2007. Makosa haya ni pamoja na utoro kazini, uzembe, kutotii mamlaka, ufanyaji kazi usioridhisha, upotevu wa mali ya mwajiri au mteja, uharibifu wa mali na kadhalika.
Kwa mujibu wa DC Makonda, Watendaji wa Ardhi walichelewa sehemu ya utatuzi wa mgogoro wa ardhi. DC Makonda amesema kuwa walikubaliana wote (yeye na Watendaji hao) kukutana sehemu ya tukio saa mbili asubuhi. Wao walifika saa tano asubuhi. Kwakuwa Watendaji hao, kimamlaka, wako chini ya Mkuu wa Wilaya na kwakuwa Watendaji hao walipokubaliana ni kama walipokea amri ya kiongozi wao, walipaswa kufika kabla au katika muda uliopangwa. Kuchelewa kwao ni kosa. Kosa husika hapo ni kutotii mamlaka. Hili ni kosa la kinidhamu, na si la kijinai. Hatua za kinidhamu ndizo zilizopaswa kuchukuliwa.
Hatua hizo ni pamoja na kusimamishwa kazi na hata kuachishwa kazi pale ambapo taratibu za kinidhamu zitafanyika na wao kukutwa na hatia ya kutenda makosa hayo ya kinidhamu. Kwa jana, DC Makonda alipaswa kuwatimua Watendaji hao na si kuwasweka rumande. Nimalizie kwa kusema kuwa,mamlaka ya Mkuu wa Wilaya kuamuru kukamatwa kwa mtu anayetenda kosa au anayedhamiria kutenda kosa au anayehatarisha amani na utulivu yanahusu makosa ya jinai tu. Sheria inayotoa mamlaka hayo ni Sheria ya Tawala za Mikoa ya mwaka 1997 chini ya kifungu cha 15 chenye vifungu vidogo 1 hadi 9. Kifungu kizima cha 15 kinahusu makosa ya jinai kwakuwa anayewekwa kizuizini anapaswa kushtakiwa mahakamani (kwa kufikishwa mbele ya Hakimu ndani ya saa 48). Kifungu cha 15 (3) kinasomeka kwa kumaanisha hivyo. Ni hiki:
(3) A person arrested under
the powers conferred by this
section shall, as soon as
Practicable, and in any case
within not more than forty-eight
hours, after he is taken into
custody, be taken before a
magistrate empowered to deal with
the case by the law for the time
being in force in relation to the
institution and prosecution of
criminal proceedings.
Kuna angalizo la kisheria, chini ya kifungu kidogo cha 9 cha kifungu hicho cha 15 cha Sheria tajwa. Angalizo lenyewe ni hili:
(9) Where a District Commissioner exercises the
power conferred on him by this section in abuse of
the authority of his office, then he, as well as any other
Person involved in procuring the District Commissioner
to exercise the power in abuse of authority, is
guilty of an offence and may be proceeded against m
accordance with section 96 of the Penal Code.
Ni hayo tu. Tukubaliane kuwa, DC Makonda alikosea kufanya alivyofanya kwakuwa makosa ya Watendaji hao ni makosa ya kinidhamu na si jinai.

Last edited by a moderator: