DC Makonda 'amekiri' kuwa lilikuwa ni suala la kinidhamu, alikosea

DC Makonda 'amekiri' kuwa lilikuwa ni suala la kinidhamu, alikosea

Ingetegemea na utetezi wao na makosa yao. Wangeweza kuonywa au kufukuzwa. Kama hakukuwa na sababu nzito za kuchelewa kwao, na baada ya vikao vya kinidhamu kwa mujibu wa sheria, hao watumishi walipaswa kuachishwa kazi

Kuachishwa kazi kwa kuchelewa kwa masaa3?

Ndo maana nasema sio kila mahali hizo sheria zinatakiwa ziamuliwe kama zilivyo !!
Muda mwingine " kanuni na utaratibu "" ufuatwe .

Viongozi watumie busara zaidi!!
 
Poor minded ni mtu yeyote anaetumia sheria na taratibu za kazi kama kinga dhidi ya uzembe na matumizi mabaya ya Ofisi. Wewe unaejua sheria za kazi inakuaje unapanga ratiba ya kikao wewe mwenyewe halafu DC anafika kwa wakati halafu wewe mtumishi mwenye kujua "sheria na taratibu" unafika kwa kuchelewa kwa saa3 i.e kutoka saa mbili asbh unafika saa 5 asbh halafu unajitapa unajua sheria za kazi. Visingizio vya kufiwa, foleni, kuuguliwa vipo kwa watumish wa Umma peke yake? Mfanyakazi wa Stanbic Bank anawahi kila siku ofisin posta, mfanyakazi wa ofisi ya Umma nae anachelewa kila siku ofisini posta lakin wote wanaishi mtaa mmoja kimara jee huko barabarani kuna folen za watumish wa Umma na wengine tofauti? Msipojinyoosha mtanyooshwa this time!

poor you. unafikiri mfanyakazi wa stanbic akichelewa anatangazwa kwenye vyombo vya habari kujitafutia sifa. hujui na hutokaa ujue, jiokoe mwenyewe!
 
Mkuu idoyo ..ww ni kilaza sana.kwanza kudharau wasio na kaz ...inaonyesha ulivyolimbuken wa kutumikishwa kazi za watu.....sasa tufanye zifuatwe taratibu ungefurahi wangefujuzw? kazi?? watumishi walio wengi(sio wote wa serikali)ni wazembe kuliko maelezo....wanyooshwe tu

msukule mwingine huyu sasa!! hata hujui kwa nini sheria zipo, binadamu sio malaika wa mungu! wacha kusubiri kuokolewa na shida zako, jiokoe mwenyewe! poor minded voter, nyie ndiyo mnashusha average IQ ya tanzania. mazuzu mnaoendeshwa kwa hisia!
 
Serikal ya kucheka cheka na Watumishi wa Umma imemaliza muda wake 5 Nov. 2015. Ccm imechukiwa kwa sababu ya Watumish wa Umma washenzi lazima wanyooshwe! Hizo nchi tunazozitumia kama Mfano watu wana nidhamu ya utendaji kazi, leo Sourthern of Sahara sifa kubwa ya watanzania ni kuchelewa kufika kwenye Vikao.

Hao wanaofanya ccm ichukiwe ndio ccm yenyewe, sheria za nchi lazima zifuatwe.
 
Hapo ni wazi bila kumung'unya maneno DC hakufanya sawa na ametumia vibaya madaraka yake. Na ieleweke pia mkuu wa wilaya yeyote sio mamlaka ya nidhamu ya mtumishi wa umma. Watumishi waliochini ya mkurugenzi wa halmashauri mamlaka Yao ya nidhamu ni mkurugenzi na walio kwa DC mamlaka ya nidhamu ni RAS.(refer PUBLIC SERVICE ACT, 2002 as amended from time to time). Kwanza kosa walilofanya hao watumishi na adhabu ya DC ni vitu tofautisana. Hapo DC kakosea na tungekuwa tunafuata utawala wa sheria vizuri na misingi ya utawala bora DC ilitakiwa awajibishwe kwa matumizi mabaya ya madaraka.

Sio jambo jema kufurahia au kushangilia uvunjaji wa sheria na taratibu hasa kwa viongozi wa umma. Ukifurahi Leo kumbuka kesho mtu huyo huyo anaweza kufanya maamuzi yatakayoigarimu serikali au wewe mwenyewe.

Tunapsawa kuwakemea viongozi wetu wanapovuka mipaka Yao ya kazi. DC angeweza kuwafukuza pale site na kumuagiza mkurugenzi wa halmashauri kuwachukulia hatu za kinidhamu (insubordination) .

We must adhere to principle of good governance .
 
Kauli zenu za kufurahia matukio zitawafikisha pabaya. Siku zote ukitaka kuleta ustawi wa jamii, hakikisha mambo ya msingi yatakayoleta ustawi wa jamii yamekuwepo. Unapodai Leo ustawi wa jamii ni nini kigezo cha huo ustaw? Unapotaka mtaalamu atoe huduma bora km za afya, je dawa zipo, cuteness kazi? Masilahi? Daktari anaishi gongolamboto kwa kuwa Nyumba za umma zimeuzwa, unataka awahi kwa kupanda ungo kuhudumia emergencies? Serikali ikusanye mapato kupitia vyanzo chake, madini, gesi, bandari, mapato ya ndani halmashauri, wafanyabiashara etc. Ukideal na daktari wakati dawa hakuna, akakutii kinafiki je mgonjwa atapona? Au mwalimu ukimshurutisha wakati hana motisha mwanao atafaulu? Mishahara yenyewe duni, Kauli zipo juu, bidhaa juu kila kitu aghali unataka mtumishi wa umna awajibije na kuleta tija? Nchi hii kwa sasa inataka makusanyo mazuri ili kuboresha huduma.
 
Mkuu HAMY-D, ameweka video ya sakata la kuswekwa ndani kwa Watendaji wa Ardhi wa Kinondoni kwa amri ya Mkuu wa Wilaya hiyo,Mhe. Paul Makonda.

Kuna angalizo la kisheria, chini ya kifungu kidogo cha 9 cha kifungu hicho cha 15 cha Sheria tajwa. Angalizo lenyewe ni hili:

(9) Where a District Commissioner exercises the
power conferred on him by this section in abuse of
the authority of his office, then he, as well as any other
Person involved in procuring the District Commissioner
to exercise the power in abuse of authority, is
guilty of an offence and may be proceeded against m
accordance with section 96 of the Penal Code.

Ni hayo tu. Tukubaliane kuwa, DC Makonda alikosea kufanya alivyofanya kwakuwa makosa ya Watendaji hao ni makosa ya kinidhamu na si jinai.



Mkuu Petro E. Mselewa naona kama unamlisha maneno DC Paul Makonda kuhusiana na hapo kwenye maneno yenye andishi nyekundu hapo chini!
Amekiri kwako au kuna mahali kaweka andishi au taarifa kwenye magazeti au ofisi yake imetoa ufafanuzi rasmi "kukiri''

Kama amefanya hivyo ni jambo njema na ustaarabu-ni kweli watumishi wanakera na hasa suala la kutokujali muda kwa Watumishi sehemu ya kazi ni ugonjwa mkubwa na kwa sasa ukiongeza na foleni hii ya Dar inakuwa kisingizio cha kutosha.

Kuna haja Kanuni ya adhabu kuhusu suala la uchelewaji liongezewa makali-Pili Dc na RC wanapokwenda site kwa shughuli za utendaji wawe wanaambatana na washauri wao wa Kisheria naamini ofisi hizi zina wanasheria .
Mfano kama hili tukio Dc angekuwa amepata ushauri mapema kabisa maana amesubiri Masaa mawili?


[h=2]DC Makonda 'amekiri' kuwa lilikuwa ni suala la kinidhamu, alikosea[/h]
 
Last edited by a moderator:
Bwana mdogo DC Makonda bado hajiamini, bado anazo njozi za kumpiga ngwara Jaji Warioba na akatunukiwa uDC, then anafikiri Rais Magufuli nae ataona amefanya kazi nzuri ampe uRC. Hii inaonyesha wazi kuwa watu wanapewa madaraka kwa njia za ushikaji au kutokana na kuchonga mdomo na majungu nasio kwa "merits". Kosa la kuchelewa anaye paswa kulichukulia hatua ni DAS na sio DC,hali kama hii inaonyesha wazi kwamba DC Makonda haelewi terms and refrence za madaraka yake na limitations zake. Sio vema ukawa na hamaki naujazo mkubwa wa hisia moyoni mwako ukakurupuka kutao maamuzi ambayo ni kinyume na utaratibu baadae unafunika uso wako na kuanza kuomba msamaha kwa subordinates wako, hii inaweza ikachangia kuanyesha udhaifu w ako kiuongozi.
DC Makonda, you can pay for school but yo can not buy CLASS, go back to school jifunze Uongozi na Utawala, madaraka ya zawadi ni magumu kuyatekeleza. Pokea madaraka ukijua unazo merits, "acha kufunga vidani vya viatu"
 
Mkuu, kuna adhabu kulingana na uzito wa kosa. Ndiyo maana ya kadhalika. Uyumwike?

Hii ya Makonda imenikumbusha kule Korea Kaskazini. Kiongozi mkuu alitoa adhabu ya kutunguliwa na kombora Waziri wa Ulinzi kwa kitendo cha kusinzia wakati yeye anahutubia.
Tukiyachekea haya tunaweza kuwa kama Korea kaskazini.
 
Hii ya Makonda imenikumbusha kule Korea Kaskazini. Kiongozi mkuu alitoa adhabu ya kutunguliwa na kombora Waziri wa Ulinzi kwa kitendo cha kusinzia wakati yeye anahutubia.
Tukiyachekea haya tunaweza kuwa kama Korea kaskazini.

Hakika Mkuu Chakaza
 
Last edited by a moderator:
Ingetegemea na utetezi wao na makosa yao. Wangeweza kuonywa au kufukuzwa. Kama hakukuwa na sababu nzito za kuchelewa kwao, na baada ya vikao vya kinidhamu kwa mujibu wa sheria, hao watumishi walipaswa kuachishwa kazi
ndugu katika utumishi wa uma kuna kamati za nidhamu ambazo zinashughulikkia masual yote ya nidhamu ya watumishi.
hakuna siku mtumishi wa uma atafukuzwa bila kusikilizwa.
lazima aitwe kwenye vikao vikae kamati isikilize wote wawili mwajiri na mwajiriwa
baada ya hapo ndio uamuzi unatolewa kuhusu adhabu anazoweza adhibiwa mtumishi ambazo zinaweza kua kupewa onyo la maandishi au mdomo, kukatwa mshahara kutokana na uzembe uliosababisha hasara kwa mwajiri, kulipwa mshahara nusu,kuzuiwa kupanda daraja, kushushwa daraja au kufukuzwa kazi, kufukuzwa kufukuzwa kazi na utumsihi.

ukifika hali ya kufukuzwa kazi serikalini ujue umeshindikana wewe yaani hawa watu wako tolerant mno.
kwa hiyo kwa swala la makonda amekurupuka balaa na nadhani ni sababu hajawahi kua mtumishi wa umma kabla ya kua mkuu wa wilaya
 
Back
Top Bottom