acer
JF-Expert Member
- Apr 4, 2012
- 1,595
- 142
UVCCM MALINYI: DC AMEVURUGA UCHAGUZI WETU
"Katika hali isiyotarajiwa mkuu wa wilaya yetu alifika kwenye ukumbi wa uchaguzi pamoja na kwamba hakuwa mgeni mwaalikwa wala mgeni rasmi,alijipa jukumu la kuwa mgeni rasmi na msimamizi wa uchaguzi wetu huu"
Hiyo ni kauli ya katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Malinyi akimshutumu mkuu wa wilaya mh Kasika kuvuruga uchaguzi wao wa vijana ambapo mwenyekiti wa halmashauri hiyo ndiye aliyekuwa mgeni rasmi, taarifa za ndani zinasema mkuu wa wilaya huyu mara baada ya kuingia aliwatoa nje makatibu wote wa UVCCM wa wilaya na Chama wilaya kwa madai ya kwamba wanatumika kwa maslahi ya mbunge wa jimbo hilo la Malinyi, lakini katika mchakato wa uchaguzi ukiendelea mkuu huyo wa wilaya alionekana kumpendelea mgombea mmoja kati ya wale watatu ambaye anaitwa Joseph.
Akieleza kwa uchungu katibu wa wazazi wilaya ,ameeleza inakuaje toka tumeanza uchaguzi kwenye mashina,kwneye kata, hakuonekana kuja hata ofisini kufahamu uchaguzi unaendeleaje leo ghafla tu anatoka huko na kutuvamia.
Kuelekea mwishoni mwa mkutano huu wa uchaguzi, bila kutimua mbio mkuu wa wilaya hii alishakana(kukunjana mashati) na katibu wa UVCCM wa wilaya aitwaye Mariam nusura amchape kofi mh mkuu wa wilaya baada ya kuanza kutoa maneno na kauli chafu mbele ya wajumbe wote dhidi ya sekretariet ,viongozi wa chama wilaya na madiwani.
Wajumbe wamelaani vikali kitendo hiki kilichofanywa na mh mkuu wa wilaya.
Imethibitika kuwa mkuu wa wilaya amekuwa na tofauti baina yake na viongozi mwenzake kupelekea kukosa ushirikiano kwa viongozi wote wa chama na serikali,waliochaguliwa na walioteuliwa pamoja na wakuu wa idara ndani ya halmashauri ya wilaya ya Malinyi.