GE2025 DC Mnzava: Wananchi wawe na amani kuna usalama Kilimanjaro, Oktoba 29 mkapige kura

GE2025 DC Mnzava: Wananchi wawe na amani kuna usalama Kilimanjaro, Oktoba 29 mkapige kura

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Leo Oktoba 22, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Godfrey Mnzava kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro wakati akifungua Semina ya Amani iliyokutanisha viongozi wa dini mbalimbali Kanda ya Kaskazini inayoongozwa na kauli mbiu "Kupiga kura ni haki yetu na Amani ya Taifa letu ni wajibu wetu".

Mnzava amesema kuwa Mkoa huo upo salama na tulivu kutokana na vyombo vya ulinzi na usalama kufanya kazi yake vizuri pamoja na wananchi kutoa taarifa kwa Serikali pale penye changamoto

"Tunaenda kwenye uchaguzi kila baada ya miaka mitano,ni takwa la kikatiba na demokrasia, Kilimanjaro hali ni nzuri wananchi wajitokeze kusikiliza sera, mipango na maono ya vyama vyao." amesema Mnzava

Amesisitiza kuwa serikali imejipanga kuhakikisha kuwa kuna kuwa na utulivu na amani ya kutosha katika zoezi la kupiga kura Oktoba 29, 2025 ili kila mwananchi mwenye sifa ya kushiriki zoezi hilo ashiriki kikamilifu


 
Back
Top Bottom