Pre GE2025 DC Momba amshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi za miradi, katika sekta ya elimu

Pre GE2025 DC Momba amshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi za miradi, katika sekta ya elimu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mkuu wa Wilaya ya Momba, Elias Mwandobo, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kutoa fedha nyingi za miradi, hasa katika sekta ya elimu.

Akizungumza katika ziara yake ya kampeni ya kuandikisha na kusajili watoto walio nje ya mfumo rasmi wa elimu (OOSC) katika Kata ya Ndalambo, Kijiji cha Chiwanda, Mwandobo alisisitiza umuhimu wa elimu nje ya mfumo rasmi wa shule kama sehemu muhimu ya kuboresha elimu nchini.

Pia soma: Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mwandobo aliongeza kusema kuwa, kuanzishwa kwa programu hiyo kunalenga kuleta mabadiliko chanya kwa watoto wengi walio nje ya mfumo wa shule na kuwawezesha kupata elimu.

Aisha Mwandobo, Alitoa shukrani kwa wananchi wa Wilaya ya Momba kwa kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi hilo, huku akiwashukuru pia wafadhili wa mradi huo, ambao ni UNICEF kwa kushirikiana na Education Above All Foundation ya Qatar, kwa msaada wao muhimu katika utekelezaji wa kampeni hii ya kuandikisha watoto.

 
huyo anasifia mwisho wa mweizi anakunja 12m kama mshahara.

ccm imeset mfumo wa kusifia. ili kuzidi kupumbaza wajinga
 
Back
Top Bottom