Mkuu wa Wilaya ya Momba, Elias Mwandobo, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kutoa fedha nyingi za miradi, hasa katika sekta ya elimu.
Akizungumza katika ziara yake ya kampeni ya kuandikisha na kusajili watoto walio nje ya mfumo rasmi wa elimu (OOSC) katika Kata ya Ndalambo, Kijiji cha Chiwanda, Mwandobo alisisitiza umuhimu wa elimu nje ya mfumo rasmi wa shule kama sehemu muhimu ya kuboresha elimu nchini.
Mwandobo aliongeza kusema kuwa, kuanzishwa kwa programu hiyo kunalenga kuleta mabadiliko chanya kwa watoto wengi walio nje ya mfumo wa shule na kuwawezesha kupata elimu.
Aisha Mwandobo, Alitoa shukrani kwa wananchi wa Wilaya ya Momba kwa kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi hilo, huku akiwashukuru pia wafadhili wa mradi huo, ambao ni UNICEF kwa kushirikiana na Education Above All Foundation ya Qatar, kwa msaada wao muhimu katika utekelezaji wa kampeni hii ya kuandikisha watoto.