Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, James Kaji, amesema hatawavumilia watumishi wazembe na kuagiza majina ya waliokwepa kushiriki maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika yawasilishwe kwake mara moja ili wachukuliwe hatua.
Kaji ametoa onyo hilo leo Jumatatu, Desemba 9, 2024, wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Viwanja vya Mashujaa, Manispaa ya Moshi, yakitanguliwa na shughuli za usafi katika makaburi ya Karanga.
Amesema uzembe wa baadhi ya watumishi wa umma unakwamisha juhudi za maendeleo zinazofanywa na Serikali na kuahidi kuchukua hatua kali dhidi yao.
"Watumishi wengi hawawajibiki mpaka wasukumwe au kushikiwa fimbo. Nchi hii ni yetu sote, sitavumilia uzembe huu. Wapo watu mitaani wanazunguka na vyeti hawana kazi, ninyi mmepata nafasi msichezee nafasi hizi. Nitachukua hatua kali kwa wote waliokwepa kushiriki maadhimisho haya kwa kuwa hiyo ni dharau," amesema Kaji.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Mwajuma Nasombe, amesema kwa kushirikiana na wadau, wamefanya usafi katika makaburi ya Karanga, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha usafi wa mji.