DC Moshi, James Kaji: Ningekuwa na mamlaka, ningetimua wote waliokosa kushiriki maadhimisho ya Uhuru

Mkuu wa Wilaya ya Moshi, James Kaji, amesema hatawavumilia watumishi wazembe na kuagiza majina ya waliokwepa kushiriki maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika yawasilishwe kwake mara moja ili wachukuliwe hatua.

Kaji ametoa onyo hilo leo Jumatatu, Desemba 9, 2024, wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Viwanja vya Mashujaa, Manispaa ya Moshi, yakitanguliwa na shughuli za usafi katika makaburi ya Karanga.

Amesema uzembe wa baadhi ya watumishi wa umma unakwamisha juhudi za maendeleo zinazofanywa na Serikali na kuahidi kuchukua hatua kali dhidi yao.

"Watumishi wengi hawawajibiki mpaka wasukumwe au kushikiwa fimbo. Nchi hii ni yetu sote, sitavumilia uzembe huu. Wapo watu mitaani wanazunguka na vyeti hawana kazi, ninyi mmepata nafasi msichezee nafasi hizi. Nitachukua hatua kali kwa wote waliokwepa kushiriki maadhimisho haya kwa kuwa hiyo ni dharau," amesema Kaji.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Mwajuma Nasombe, amesema kwa kushirikiana na wadau, wamefanya usafi katika makaburi ya Karanga, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha usafi wa mji.
Hawa watu wakiamka wanevimbiwa basi hujiropokea tu watakavyo bila kutafakari athari ya matamshi yao
 
Msameheni tu huyu,ni mtumiaji wa ile dozi ya nanii.
 
Propaganda sio swala la nguvu, ni swala la persuasion, it’s very tactical and very expensive.

Tanzania bado
 
Msaki Ringo Masawe na Maro Mushi Nkya hawakuja kusafisha makabur Katanga Anza nao. Umeambiwa hawana ndugu wa kusafisha makaburi yao hadi ya Katanga Tu?
 
Mkuu wa Wilaya ya Moshi, James Kaji, amesema hatawavumilia watumishi wazembe na kuagiza majina ya waliokwepa kushiriki maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika yawasilishwe kwake mara moja ili wachukuliwe hatua.

Kaji ametoa onyo hilo leo Jumatatu, Desemba 9, 2024, wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Viwanja vya Mashujaa, Manispaa ya Moshi, yakitanguliwa na shughuli za usafi katika makaburi ya Karanga.

Amesema uzembe wa baadhi ya watumishi wa umma unakwamisha juhudi za maendeleo zinazofanywa na Serikali na kuahidi kuchukua hatua kali dhidi yao.

"Watumishi wengi hawawajibiki mpaka wasukumwe au kushikiwa fimbo. Nchi hii ni yetu sote, sitavumilia uzembe huu. Wapo watu mitaani wanazunguka na vyeti hawana kazi, ninyi mmepata nafasi msichezee nafasi hizi. Nitachukua hatua kali kwa wote waliokwepa kushiriki maadhimisho haya kwa kuwa hiyo ni dharau," amesema Kaji.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Mwajuma Nasombe, amesema kwa kushirikiana na wadau, wamefanya usafi katika makaburi ya Karanga, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha usafi wa mji.
Amelewa CHIMPUMU sio bureee 🤣🤣😂😂😂
 
Wengine tuliamua kuadhimisha kwa kwenda kusali kanisani na misikitini kuliombea taifa ili mpunguze ukatili wenu dhidi yetu.
 
Amesema uzembe wa baadhi ya watumishi wa umma unakwamisha juhudi za maendeleo zinazofanywa na Serikali na kuahidi kuchukua hatua kali dhidi yao.
Kwamfano kuto kuhudhuria kwenye hayo maadhimisho kunakwamisha maendeleo Gani ?
 
Ila viongozi wetu 😂😂😂😂
 
mweupe sana huyu jamaa kichwani, anapenda wadada tu. Sishangai kwa hiki anachozungumza, ndio maana akawa demoted kutoka kamishna jenerali dcea hadi dc. Naona mama alipata file lake.
 
Uyu kwa kauli hizi kwa watumishi astahili ata dakika 10 kuwa ofisini , Hajui ata maana ya uhuru, kila mtu anahaki kuazimisha sherehe tajwa kwa matakwa yake ,ulipatika uhuru ili watu wawe huru, sasa analeta ujinga gani wa kupangia watumishi cha kufanya . Hawa upataje nafasi kama izi?
upepo wa kumbeba kila msukuma na watu wa kanda ya ziwa wakati wa 2015 -2020 ndio uliwabeba watu kama hawa mkuu.
 
Back
Top Bottom