Mkuu wa wiyala ya Ilala Edward Mpogolo amemshukuru Rais Dkt. Samia kwa kuendelea kutoa pesa Halmashauri ya Ilala na kuweza kutekeleza Miradi mbali Mbali katika wilaya hiyo
Mpogolo amesema katika kipindi cha miaka 4 ya Rais Dkt. Samia zaidi ya Bilioni 317 zimetolewa kwenye wilaya ya Ilala na kutumika kwenye Miradi mbali mbali ya maendeleo
Mpogolo amesisitiza fedha zilizopokewa ni nyingi na zinaonyesha matokeo chanya katika miradi ya maendeleo kwa wananchi wilayani Ilala.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo ameeleza kutokana na kazi kubwa aliyofanya Rais wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan kuna kila sababu ya kumpa kura za kutosha katika uchaguzi wa mwezi wa kumi mwaka huu.
Kwa wale mliopo Ilala mtuambie nini mmekiona katika miaka minne zaidi ya barabara ya mwendokasi ambayo imesimama kwa muda mrefu. Watuambie hizo bilioni 337 zimefanya nini kwa wananchi?