Responded DC Mpogolo: Nyaya za mawasiliano Kariakoo zimetanda kama buibui

Responded DC Mpogolo: Nyaya za mawasiliano Kariakoo zimetanda kama buibui

informer 06

Senior Member
Joined
May 11, 2024
Posts
184
Reaction score
170
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema ufungaji holela wa nyaya za mawasiliano katika eneo la Kariakoo na baadhi ya maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam unaathiri mandhari ya Jiji, huku ukisababisha changamoto katika upitishaji wa mizigo kwa magari makubwa na ufikishaji wa vifaa vya zimamoto wakati wa dharura.
IMG_3620.jpeg
Akizungumza Oktoba 10, 2026, baada ya kukamilika kwa zoezi la usafi lililoratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Mpogolo amesema hali hiyo ni changamoto inayohitaji ufumbuzi wa haraka.

Pia soma ~ Ufungaji holela wa nyaya za intaneti Kariakoo si rafiki kwa mandhari ya Jiji

Amesema nyaya zinazofungwa holela na zile zinazoachwa chini baada ya kuharibika au kuondolewa zinachafua mazingira, huku baadhi zikiziba mitaro na kuathiri miundombinu ya maji taka.

Amesema ili kukabiliana na hali hiyo, wataiandikia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ambayo ina jukumu la kusimamia sekta ya mawasiliano nchini, ili ichukue hatua dhidi ya kampuni zinazofunga nyaya bila kuzingatia utaratibu unaotakiwa.

Akizungumza na viongozi waliohudhuria zoezi hilo, Mpogolo amemuomba Mkurugenzi wa Jiji kushirikiana na ofisi yake kuwasiliana rasmi na TCRA ili hatua zichukuliwe dhidi ya kampuni zinazochangia uchafuzi huo.

“Nikuombe Mkurugenzi wetu wa Jiji, uiandikie TCRA. Tuiandikie barua rasmi tukiwataka wawaandikie na kuwaonya taasisi na kampuni binafsi zinazofikisha huduma za mawasiliano katika maeneo mbalimbali. Zinachafua sana mazingira ya Jiji la Dar es Salaam. Unakuta waya kila mahali. Hata watu wetu wanapoenda kufanya kazi wanashindwa kufanya kazi,” amesema Mpogolo.
IMG_3615.jpeg
Ameongeza kuwa hali ya nyaya hizo katika eneo la Kariakoo inafanana na utando wa buibui.

“Lakini ukienda Kariakoo, ni kama unaingia kwenye utando wa buibui. Unaweza kufikiri buibui ametanda Kariakoo, kumbe ni nyaya za mawasiliano,” amesema.

Wadau wengine waige mfano wa TTCL
Aidha, ameipongeza TTCL kwa juhudi zake katika maeneo ambayo miundombinu ya mawasiliano, ikiwamo mkongo wa mawasiliano, imepitishwa kwa utaratibu unaofaa.

Hata hivyo, ameitaka kampuni hiyo kuendelea kuhakikisha kuwa maeneo yanayochimbwa kwa ajili ya kupitisha miundombinu ya mawasiliano yanaachwa katika hali nzuri ili kulinda mazingira na kurahisisha matumizi ya maeneo hayo na wananchi.
IMG_3618.jpeg
Zoezi la usafi ambalo limeanza majira ya saa moja asubuhi pia lilihusisha utoaji wa vifaa vya usafi vilivyotolewa na TTCL ikielezwa kuwa ni sehemu ya kuunga mkono kampeni za usafi zinazoendelea katika Jiji la Dar es Salaam.


Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeungana na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Edward Mpogolo, katika zoezi la usafi wa mazingira lililofanyika eneo la Posta, Dar es Salaam.
IMG_3619.jpeg
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mkurugenzi wa Ufundi wa TTCL, Mhandisi Cecil Francis, amesisitiza dhamira ya Shirika ya kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuhamasisha usafi na utunzaji wa mazingira.

Mpogolo ameipongeza TTCL Kwa kushiriki kikamilifu na kuchangia vifaa mbalimbali vya usafi, vikiwemo fagio, viatu vya usafi, barakoa na Majaba ya taka (Dustbin).
 
Back
Top Bottom