PostGE2025 DC Mpogolo: Wamekuja watu wa hovyo, wakatumia bodaboda kuhalalisha haramu yao — lindeni amani

PostGE2025 DC Mpogolo: Wamekuja watu wa hovyo, wakatumia bodaboda kuhalalisha haramu yao — lindeni amani

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amewataka viongozi wa Maafisa Usafirishaji na Wamachinga kuunda timu maalum itakayozunguka katika vijiwe vya bodaboda na maeneo ya wafanyabiashara kutoa elimu juu ya umuhimu wa kudumisha amani.

Hayo ameyabainisha leo katika kongamano la Maafisa Usafirishaji na Wamachinga wa Wilaya ya Ilala lililofanyika katika Ukumbi wa Drimp Ilala Boma jijini Dar es Salaam, Ambapo Mpogolo amesema amani ni msingi wa maendeleo ya taifa na kila mwananchi anao wajibu wa kuitunza.

Soma pia > Bodaboda na Machinga Dar: Desemba 9 hatufungui biashara

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Wilaya ya Ilala Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi (RPC) ACP. Yustino Mgonja ameahidi kuendelea kushirikiana na viongozi wa maeneo mbalimbali kuhakikisha elimu ya kujenga amani inawafikia vijana na makundi yote ya wafanyabiashara pia amesema Jeshi la Polisi litaongeza doria na mikutano ya kijamii ili kuimarisha uhusiano na wananchi.

Nao viongozi wa Maafisa Usafirishaji na Wamachinga wameahidi kushirikiana kwa karibu na Serikali katika kutekeleza maelekezo hayo, wakisema watahakikisha wanawafikia bodaboda na wafanyabiashara katika vituo mbalimbali kwa kutoa elimu ya amani kwani ni muhimu kwa sababu sekta ya usafirishaji na biashara ndogondogo ina watu wengi, hivyo kuwa sehemu sahihi ya kuimarisha ushirikiano na ustawi wa jamii.

 
Eti 'Maafisa Usafirishaji' ! 😆😂🤣 Matumizi mabaya ya neno Afisa.
 
Hawa watu ni wameoza ubongo... Kuwepo kwa bodaboda wengi hivyo ni kielelezo cha kufeli kwa Serikali
 
Back
Top Bottom