DC Mpogolo: Watu wenye fedha ambao hutumia vibaya pesa zao kununua migogoro ya ardhi

DC Mpogolo: Watu wenye fedha ambao hutumia vibaya pesa zao kununua migogoro ya ardhi

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Mkuu wa Wilaya ya Ilala mkoani Dar es Salaam, Edward Mpogolo, amesema migogoro ya ardhi ni changamoto ya kimataifa inayohitaji suluhu endelevu, huku akibainisha kuwa mabaraza ya ardhi ya kata ni nguzo muhimu katika upatanishi wa wananchi.

“Wapo watu wenye fedha ambao hutumia vibaya pesa zao. Akiona mgogoro kati ya watu wawili, yeye anaamua kununua ule mgogoro. Mfano, Wilberforce unagombana na mtu mwingine, akaja mtu akasema ‘hii kesi ni yangu, nitapambana nayo kwa pesa.’ Huo ndiyo ukweli unaosababisha changamoto kubwa kwenye ardhi,” ameongeza.

 
Back
Top Bottom