PostGE2025 DC Msando: Hakuna mtego kwa Askofu Gwajima, kufungulia kanisa lake

PostGE2025 DC Msando: Hakuna mtego kwa Askofu Gwajima, kufungulia kanisa lake

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Serikali imesema hakuna mtego wowote uliowekwa kwa Askofu Dkt. Josephat Gwajima, unaotokana na kufunguliwa kwa Kanisa la Ufufuo na Uzima analoliongoza

Kauli hiyo ya serikali imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Dar es Salaam Wakili Albert Msando kwaniaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi George Simbachawene alipofika Kanisani hapo leo, Jumanne Novemba 25.2025, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba aliyotoa Novemba 24 mwaka huu yaliyotaka kufunguliwa kwa Kanisa hilo ili waumini wake waendelee kufanya ibada huku likiwa kwenye uangalizi maalum

Wakili Msando amelazimika kutoa ufafanuzi huo kutokana na taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya kujamii kuwa huenda kufunguliwa huko ni sehemu ya mtego wa kutaka kumkamata Askofu Dkt. Josephat Gwajima

Aidha, Wakili Msando amewaelekeza viongozi wa Kanisa hilo kufanya ukaguzi na kufanya ulinganifu tangu walivyoondoka Kanisani hapo hadi sasa, na kama wataona kuna kasoro yoyote wasisite kwenda Ofisini kwake kumpatia taarifa.

 
Mmmh huo upendo mbona unanitisha ? HUU MTEGO HUU
 
Huo uangalizi ni uangalizi wa kitu gani?...kwani sababu ya kulifungia kanisa zilikuwa zipi?....
Taifa limejaa mazezeta sana...
 
Mrudisheni kwanza Chaula aliechoma picha ya Samia ndio tutajua ya Gwajima sio mtego. Damu mlizokunywa hazijatosha tu?🤕🤕🤕
 
Jasusi la mbinguni linawazoom tu 😂😂😂

IMG-20251024-WA0076.jpg
 
Back
Top Bottom