PostGE2025 DC Msando: Kamera za CCTV Goba ziling'olewa na waandamanaji Oktoba 29

PostGE2025 DC Msando: Kamera za CCTV Goba ziling'olewa na waandamanaji Oktoba 29

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Albert Msando, ameingilia kati na kutolea ufafanuzi sintofahamu iliyotawala miongoni mwa wakazi wa Goba kuhusu kuondolewa kwa kamera za usalama (CCTV) katika makutano ya barabara za Goba Center na Goba Njia Nne.

Kamera hizo, ambazo zilikuwa ni matunda ya mpango wa kuboresha usalama na usimamizi wa trafiki ulioanzishwa na DC Msando mwezi Juni mwaka jana, zilitoweka katika kipindi cha miezi miwili iliyopita, hali iliyozua mijadala mizito mitandaoni.

Kufuatia hofu na dhana zilizoenezwa kuwa kamera hizo ziliondolewa na Jeshi la Polisi ili kuficha ushahidi wa vurugu za Oktoba 29, 2025, DC Msando amebainisha ukweli wa jambo hilo ambapo amesema kuwa kamera hizo hazikuondolewa na Serikali, bali ziling’olewa na kuharibiwa na watu walioshiriki katika maandamano na vurugu za Oktoba 29. Amefafanua kuwa polisi wasingeweza kung'oa kamera hizo kwani zilikuwa ni nyenzo muhimu ya kuwasaidia kuwatambua waliofanya uhalifu siku hiyo.

Licha ya uharibifu huo, DC Msando amewahakikishia wananchi kuwa jitihada za kuimarisha usalama wa barabara na nidhamu ya madereva bado ni kipaumbele.

Amesema kuwa, tofauti na awali ambapo aliweka kamera hizo kupitia jitihada zake binafsi, sasa kuna mpango mkubwa wa Serikali kuu wa kufunga kamera za usalama katika maeneo yote muhimu nchini, kama ilivyotekelezwa jijini Dodoma.
 
Hivi kuna watu wanamuamini kiongozi yeyote wa Serikali siku hizi?

Hawa hawa wanaootuambia wanakula nyama DODOMA kusherehekea mauwaji ya raia?
Punguzeni kutengeneza habari za uongo zenye lengo la uchonganishi. Waziri Mkuu hakusema wanakula nyama Dodoma kusherehekea mauaji, umemnukuu tofauti na alichosema.

Uhuru mwingi wa kuongea huleta uzushi na upotoshaji, epukeni hii tabia inakuja kuleta machafuko ya kisiasa inapoachwa ikaota mizizi.
 
Uzuri wa uhuru wa kuongea unakupa hata wewe haki ya kutuambia alichosema.

Amandla...
 
Basi wewe ungetuambia alichosema huyo Waziri Mkuu FEKI!
 
Uzuri wa uhuru wa kuongea unakupa hata wewe haki ya kutuambia alichosema.

Amandla...
Alikuwa anaongelea namna wapambe wanavyouana wakati wao wanasiasa wanapokutana Dodoma hawaangalii huyu CCM huyu CHADEMA wanakula nyama wakiwa kitu kimoja.

Mpambe anakuwa tayari kufa wakati mwanasiasa anajenga urafiki na wanasiasa wenzake, alikuwa anawapiga madongo chawa wa wanasiasa.
 
Lakini ninadhani rekodi za walioondoa hizo camera zipo kwenye computer ambayo isingewezekana wahalifu wa 29th Oct kuifikia. Mhe DC pitia rekodi za siku hiyo ukamate hao wahuni. Au walivaa kininja?
 
Yaani hapo rekodi zipo Kwa muliro wanacheki video tu😄😄.
Mnashangaa watu wanapotea tu
 
Alikuwa anaongelea namna wapambe wanavyouana wakati wao wanasiasa wanapokutana Dodoma hawaangalii huyu CCM huyu CHADEMA wanakula nyama wakiwa kitu kimoja.

Mpambe anakuwa tayari kufa wakati mwanasiasa anajenga urafiki na wanasiasa wenzake, alikuwa anawapiga madongo chawa wa wanasiasa.
Kuna wakati ilikuwa hivyo. Kuanzia 2015 hao wapinzani wakula nao nyama Dodoma walitoka wapi? Labda wale waliopewa viti maalum vya Chadema. Ule umoja aliouzungumzia ulikuwepo kabla ya Lissu kupigwa risasi na wapinzani kugeuzwa maadui. Kuanzia hapo haupo. Na sasa ndio kabisa.

Amandla...
 
Kwaio na NVR zilichukuliwa na waandamanaji, hawa wataki kutoa ushaidi tu
 
Back
Top Bottom