Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Saad Mtambule, Juni 30, 2026, akihojiwa Kupitia Wasafi FM, amesema uchunguzi kuhusu vipeperushi vilivyosambazwa wilayani humo unaendelea kwa umakini mkubwa ili kubaini waliohusika.
"Mimi ninachotambua, ninachojua ni kwamba uchunguzi seriously unaendelea, kubaini ni akina nani. Na nina imani kwa ueledi mkubwa wa Jeshi letu la Polisi, watapatikana tu. Alafu watatupatia taarifa kwa sababu vipeperushi vile watu wengi wameviona, na jumbe zilizoko pale ni za kuchafua, zenye kuleta vurugu kwenye wilaya yetu ya Kinondoni. Kwa hiyo watakapokamilisha hiyo, watatuambia, na pengine tunaweza tukaja hata hapa na RPC tukazungumza hiyo ni nini hasa ambacho wamebaini na mwelekeo wa kisheria ukoje."