Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Zainab Abdallah ametoa pikipiki kwa Vijana wa UVCCM Mkoa wa Tanga ili zitumike na Vijana kusikiliza na kutatua kero za Vijana, kusemea kazi nzuri zinazo fanywa na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan lakini pia zitumike kuhamasisha zoezi la kuboresha taarifa kwenye daftari la kudumu la Mpiga kura.
DC Zainab Abdallah ametoa pikipiki hizo kwenye Kongamano la UVCCM Wilaya ya Muheza lililohudhuriwa na Mgeni rasmi Waziri Ridhiwan Kikwete na Naibu Waziri Hamis Mwinjuma (FA) ambapo DC Zainab amechangia pia vifaa vya ujenzi wa jengo la Katibu wa UVCCM Wilaya ya Muheza pamoja na kuchangia Tsh. 5,000,000 kwa ajili ya gharama za ufundi ili kuhakikisha nyumba hiyo inakamilika kwa wakati na kutoa fursa kwa Mtendaji wa UVCCM kufanya kazi katika mazingira bora.
DC Zainab amesema "Nimefanya kazi Mkoa wa Tanga kwa miaka saba, Mimi ni zao la UVCCM, nina wajibu wa kuacha alama ya kudumu katika Mkoa huu, hivyo kwa mapenzi makubwa nachangia pikipiki 10 kwa Wilaya zote za Mkoa wa Tanga zikawasaidie Watendaji wa Jumuiya yetu"
"Pikipiki hizi pamoja na majukumu mengine zikatumike kwenda kusikiliza na kutatua kero za Vijana, zikatumike kusemea kazi nzuri zinazo fanywa na Mwenyekiti wetu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan lakini pia zikatumike kuhamasisha zoezi la kuboresha taarifa kwenye Daftari la Kudumu la Uchaguzi, ambalo kwa Tanga zoezi hili linatarajiwa kuanza February 13, 2025, twendeni tukafanye kazi ya kukiletea ushindi Chama Cha Mapinduzi na Viongozi wake"
Kongamano hilo limehuhudhuriwa pia na Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa, Shamira Mshangama ambaye licha ya kutoa elimu kwa Vijana wenzake kuhusu fursa na uongozi kwa Vijana pia amewapa UVCCM Muheza Cherehani tano ili kuunga mkono mradi wa Vijana wa Wilaya hiyo.
Soma, Pia: