Pre GE2025 DC Muheza akabidhi Pikipiki 10 kwa UVCCM Tanga, ahamasisha Ushindi wa CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ni jambo jema na la kuigwa na wengine.
DC yuko kwenye ofisi za umma unagawa vifaa kwa chama chake?! Alishindwa nini kumpa mwenyekiti wa ccm wa wilaya agawe hizo pikipiki? Huu uchawa wa kipuuzi utaisha siku ccm inatoka madarakani.
 
DC yuko kwenye ofisi za umma unagawa vifaa kwa chama chake?! Alishindwa nini kumpa mwenyekiti wa ccm wa wilaya agawe hizo pikipiki? Huu uchawa wa kipuuzi utaisha siku ccm inatoka madarakani.
Wivu tu ndio unakusumbua
 
Tukisema chama cha ccm kinafisadi inchi katika kivuli cha ruzuku tuelewane wakuu.

Yani mtu anateuliwa kama mkuu wa Wilaya, mkuu wa mkoa , mshahara analipwa na kodi za wananchi ila unamkuta anafanya kazi za chama ,amevaa masare ya chama hata aibu hana na anaona yupo sawa

Mwenyekiti wa chama mkoa / wilaya anatosha fanya kazi za chama ,hizi nafasi za wakuu wa mkoa na wilaya zilitakiwa zitangazwe watu waombe wenye sifa bila kutochanganyikana na siasa.

Yani ulipwe mshahara kwa kodi za wananchi wote wenye vyama na wasio na vyama alafu ,daily upo kwenye majukwaa ya chama kufanya siasa badala ya kuhudumia watu.

Alafu utasikia ccm wanasema inatumika ruzuku, je mshahara walipwao D.C na ma RC ni kutokana na ruzuku ya chama? Kama sivyo kwa nini wajihusishe na siasa za ccm .

Ngoja uchaguzi uje , ccm lazima mkae pembeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…