DC Odunga akata rufaa, apinga kutoa Sh7 milioni za matunzo ya mwanaye

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga amekata rufaa Mahakama ya Wilaya Ilala akipinga hukumu ya Mahakama ya Mwanzo ya Ukonga.

Katika hukumu hiyo, Odunga alitakiwa kutoa Sh7 milioni kama nusu ya gharama za matunzo aliyotumia mkewe, Medilina Mbuwuli kumsomesha mtoto wao kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita. Odunga alifungua kesi kumtaliki mkewe lakini mahakama ililikataa ombi hilo, badala yake ikamtaka alipe kiasi hicho cha fedha.

Jana, Medelina alikwenda Mahakama ya Ukonga kujua utekelezaji wa hukumu hiyo na kukumbana na rufaa ya Odunga. Katika hukumu ya Ukonga, Odunga pia alitakiwa kutoa Sh100,000 kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya mwanaye. Kwa mujibu wa rufaa hiyo ambayo nakala yake ilipokelewa na Mbuwuli Novemba 5, itatajwa mahakamani hapo Novemba 19.

Katika maelezo ya kukata rufaa, Odunga alidai kuwa hakimu aliyesikiliza kesi yake dhidi ya Medilina alifanya kosa kutamka amlipe Sh7 milioni. Alisema hakimu huyo alifanya kosa kwa kutokutoa talaka na kubainisha kuwa ana imani ndoa yake haipo.

Katika hukumu hiyo iliyotolewa Oktoba 18 na Hakimu Christina Luguru baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na pande zote mbili alisema mdaiwa aliiomba mahakama kuwa Odunga atoe nusu ya Sh13 milioni ambazo alitumia kumhudumia mtoto wao na aendelee kuwatunza yeye na mwanaye kwa kuwa bado ni mkewe.

Hakimu Luguru alisema sheria ya ndoa kifungu cha 63 inaeleza pamoja na kifungu cha 129 ni jukumu la baba kutunza mke na mtoto. Alisema kwa ushahidi uliotolewa kwenye kesi hiyo, umeonyesha mtoto wao bado anasoma na mdai hakuwa akitoa matunzo hadi kupelekwa polisi.

Odunga hakuwa na ushahidi wowote kuonyesha alikuwa akilipa ada ila mdaiwa alipeleka risiti za ada mahakamani zikionyesha alilipa Sh14 milioni.

Katika kesi hiyo, mwanamke huyo alikuwa anadai kuwa mumewe hajawahi kutoa matunzo ya mtoto wao wa kike mwenye miaka 18 tangu akiwa chekechea hadi sasa yupo kidato cha sita.

Alisema licha ya mumewe kutotoa matunzo hayo, hayupo tayari kupewa talaka kwa sababu ndoa yao ni takatifu ya kanisani na bado anampenda mume wake na kwamba anajua hizo ni changamoto tu zimempitia.

Chanzo: Mwananchi
 
Safiiiiiii mwanamke pambana sana, usiachie hiyo ndoa, sbb nimeangalia kwa makini mwanaume ndio mwenye kosa hapo na kiburi chote sbb kapewa u DC na akitolewa u DC michepuko atakuwa hana, kiburi kitaisha, fedha zitapungua na heshima ya ndoa itarudi, kuna watu wakipata mafanikio kidogo tu anaona mke au mume wake hana maana kabisaaaa yaani alioelewa au kumuoa kwa makosa.. Yote sbb kasahau katoka wapi, kisa kiburi cha fedha.
 
Alipe sh.7M,halafu bado aendelee kulipa laki kila mwezi,na huyo mke wake anadai anampenda sana Odunga,hizo ni changamoto tu,na hataki talaka.Ukisikia ya dunia,hayo ndiyo yadunia sasa,jamaa anapitia kipindi kigumu sana.
 
Mama huyu ana roo mbaya too much a kwamaaana anamuharibia jamaaa. UDC na jpm huwenda atamvaa huyu jamaaa nakumfuta udc
 
Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga amekata rufaa Mahakama ya Wilaya Ilala akipinga hukumu ya Mahakama ya Mwanzo ya Ukonga.

Katika hukumu hiyo, Odunga alitakiwa kutoa Sh7 milioni kama nusu ya gharama za matunzo aliyotumia mkewe, Medilina Mbuwuli kumsomesha mtoto wao kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita. Odunga alifungua kesi kumtaliki mkewe lakini mahakama ililikataa ombi hilo, badala yake ikamtaka alipe kiasi hicho cha fedha.

Jana, Medelina alikwenda Mahakama ya Ukonga kujua utekelezaji wa hukumu hiyo na kukumbana na rufaa ya Odunga. Katika hukumu ya Ukonga, Odunga pia alitakiwa kutoa Sh100,000 kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya mwanaye. Kwa mujibu wa rufaa hiyo ambayo nakala yake ilipokelewa na Mbuwuli Novemba 5, itatajwa mahakamani hapo Novemba 19.

Katika maelezo ya kukata rufaa, Odunga alidai kuwa hakimu aliyesikiliza kesi yake dhidi ya Medilina alifanya kosa kutamka amlipe Sh7 milioni. Alisema hakimu huyo alifanya kosa kwa kutokutoa talaka na kubainisha kuwa ana imani ndoa yake haipo.

Katika hukumu hiyo iliyotolewa Oktoba 18 na Hakimu Christina Luguru baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na pande zote mbili alisema mdaiwa aliiomba mahakama kuwa Odunga atoe nusu ya Sh13 milioni ambazo alitumia kumhudumia mtoto wao na aendelee kuwatunza yeye na mwanaye kwa kuwa bado ni mkewe.

Hakimu Luguru alisema sheria ya ndoa kifungu cha 63 inaeleza pamoja na kifungu cha 129 ni jukumu la baba kutunza mke na mtoto. Alisema kwa ushahidi uliotolewa kwenye kesi hiyo, umeonyesha mtoto wao bado anasoma na mdai hakuwa akitoa matunzo hadi kupelekwa polisi.

Odunga hakuwa na ushahidi wowote kuonyesha alikuwa akilipa ada ila mdaiwa alipeleka risiti za ada mahakamani zikionyesha alilipa Sh14 milioni.

Katika kesi hiyo, mwanamke huyo alikuwa anadai kuwa mumewe hajawahi kutoa matunzo ya mtoto wao wa kike mwenye miaka 18 tangu akiwa chekechea hadi sasa yupo kidato cha sita.

Alisema licha ya mumewe kutotoa matunzo hayo, hayupo tayari kupewa talaka kwa sababu ndoa yao ni takatifu ya kanisani na bado anampenda mume wake na kwamba anajua hizo ni changamoto tu zimempitia.

Chanzo: Mwananchi
Hiyo ni tabia ya wanaCCM wote, ndio wanao sababisha watoto uyatima mtaani
 
Apewe m7 halafu laki kila mwezi atanue na kibenten. Hapaana.
 
We jamaa kumbe hata hufatilii ungekaa kimya basi.
DC tayari ana mke wake mwingine tena wa ndoa sio hilo gudegude linalotaka kutunzwa na pesa juu.

Hawana uhusiano wowote wakimapenzi miaka mingi sana sasa hivi sheria ya ndoa (wazee wa defamation) watanisaidia inasema mwanaume na mwanamke wakiishi nyumba moja kimapenzi tayari ni mme na mke hao.
Hawa wana miaka ya kutosha hawana uhusiano wowote je sheria inasemaje?

Hilo zuzu linalotaka pesa natamani ingekuwa ni mimi angeifurahia show sitoi hata senti 5

Soma hapo vizuri huyo mwanamke ni mke wake wa ndoa ya kanisani, ndio maana DC alipeleka maombi ya rufaa apate talaka, sasa kama hajamuoa talaka ya nini? Soma vizuri hao wamefunga ndoa kanisani
 
Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga amekata rufaa Mahakama ya Wilaya Ilala akipinga hukumu ya Mahakama ya Mwanzo ya Ukonga.

Katika hukumu hiyo, Odunga alitakiwa kutoa Sh7 milioni kama nusu ya gharama za matunzo aliyotumia mkewe, Medilina Mbuwuli kumsomesha mtoto wao kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita. Odunga alifungua kesi kumtaliki mkewe lakini mahakama ililikataa ombi hilo, badala yake ikamtaka alipe kiasi hicho cha fedha.

Jana, Medelina alikwenda Mahakama ya Ukonga kujua utekelezaji wa hukumu hiyo na kukumbana na rufaa ya Odunga. Katika hukumu ya Ukonga, Odunga pia alitakiwa kutoa Sh100,000 kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya mwanaye. Kwa mujibu wa rufaa hiyo ambayo nakala yake ilipokelewa na Mbuwuli Novemba 5, itatajwa mahakamani hapo Novemba 19.

Katika maelezo ya kukata rufaa, Odunga alidai kuwa hakimu aliyesikiliza kesi yake dhidi ya Medilina alifanya kosa kutamka amlipe Sh7 milioni. Alisema hakimu huyo alifanya kosa kwa kutokutoa talaka na kubainisha kuwa ana imani ndoa yake haipo.

Katika hukumu hiyo iliyotolewa Oktoba 18 na Hakimu Christina Luguru baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na pande zote mbili alisema mdaiwa aliiomba mahakama kuwa Odunga atoe nusu ya Sh13 milioni ambazo alitumia kumhudumia mtoto wao na aendelee kuwatunza yeye na mwanaye kwa kuwa bado ni mkewe.

Hakimu Luguru alisema sheria ya ndoa kifungu cha 63 inaeleza pamoja na kifungu cha 129 ni jukumu la baba kutunza mke na mtoto. Alisema kwa ushahidi uliotolewa kwenye kesi hiyo, umeonyesha mtoto wao bado anasoma na mdai hakuwa akitoa matunzo hadi kupelekwa polisi.

Odunga hakuwa na ushahidi wowote kuonyesha alikuwa akilipa ada ila mdaiwa alipeleka risiti za ada mahakamani zikionyesha alilipa Sh14 milioni.

Katika kesi hiyo, mwanamke huyo alikuwa anadai kuwa mumewe hajawahi kutoa matunzo ya mtoto wao wa kike mwenye miaka 18 tangu akiwa chekechea hadi sasa yupo kidato cha sita.

Alisema licha ya mumewe kutotoa matunzo hayo, hayupo tayari kupewa talaka kwa sababu ndoa yao ni takatifu ya kanisani na bado anampenda mume wake na kwamba anajua hizo ni changamoto tu zimempitia.

Chanzo: Mwananchi
Bado anampenda au anapenda cheo chake? Yani baada ya odunga kupata cheo Mke amebadili mawazo sasa anampenda mume hizo ni changamoto tu khaaaaa
 
CCM wana hizi tabia sana, wanaongoza kwa kujaza watoto wa miaani ndio maana wanapinga hawa ombaomba kuwekwa vituoni
 
hajawahi kutoa matunzo wala kumlipia ada mtoto wake lazima alipe hizo pesa kwa sababu uwezo wa kutunza watoto anao
 
Back
Top Bottom