Elections 2015 DC Paul Makonda avundua madudu ya Magufuli katika ujenzi wa barabara Kinondoni

Elections 2015 DC Paul Makonda avundua madudu ya Magufuli katika ujenzi wa barabara Kinondoni

unakurupuka kama umeng'atwa na nyigu! hizo ni barabara za manispaa na sio za tanroads. we ndio walewale wanaofanya JF kuwa kama kijiwe cha wapiga parapa:mvutaji:
 
Moja ya changamoto kubwa ni kuelimisha umma kwamba sekta ya barabara imegawanywa. Kuna barabara kuu ziko chini ya TANROADS na ndio portifolio ya Magufuli.

Na kuna barabara ndogondogo ziko chini ya Halmashauri. Ni portifolio ya Waziri Mkuu.

Kwa hiyo bwana Lowassa anapojisifia Shule za Kata tunaweza kuangalia tu je portifolio yake ilikuwaje across the board (including barabara za halmashauri).

Bwana Makonda kwamba ni stalwart opposer wa Mamvi anajulikana. Hii ni ushahidi wa kwamba mfumo sio tatizo, tatizo ni watu. Ndani ya mfumo tuna watu makini kama Makonda.

Badili tabia, usibadili chama.

Tabia chafu hata uende wapi utaenda nayo!
 
Barabara zilizoko ndani ya manispaa yotote tenda ya ujenzi hutolewa na wakurugenzi chini ya mwavuli wa kamati ya miundombinu na Kamati ya fedha na mipango ya manispaa ambayo inakuwa na mbunge wa jimbo,madiwani,meya na mwanasheria wa manispaa husika
Barabara hizi zote kabla ya kujengwa huhitaji kwanza tenda itangazwe na manispaa husika..
Baada ya kutangaza tenda wale bidders huoaswa kulipa 10% ya faida ya ujenz na baada ya hapo wakianza kazi hulipwa robo robo mara nne..: Kilichotokea katika barabara ya Biafra na barabara inayotokea sinza ambapo kuna ubadhirif ulifanyika ni suala ambalo lipo ndani ya uongoz wa manispaa ya kinondoni
: N sio sawa hili jambo kumuunganisha mh RAIS..

Maana tenda hakutoa yeye na hao wanaohusika sio TANROADS ila ni private firms..

Kazi ya DC ni kuhakikisha ilani ya ccm imetekelezwa kwa asilimia mia. Na alichokifanya DC makonda ni kutimiza wajibu wake. Hili suala Wizara haihusiki kabisa ila lipo chini ya control ya manispaa ya kinondoni Ndio maana hakuiomba wizara ya ujenz kuleta ripoti ila aliiomba manispaa ilete taarifa hizo. Maana yeye sio sehem ya halmashauri ya manispaa ila ni mtu alietumwa kusimamia ilani ya
Chama katika mkoa au wilaya husika na hili suala has nothing to do with Magufuli.

Barabara hizo wakati zinazinduliwa MH JPM alikuwa hajawa waziri wa Ujenzi

Nikuombeni tusiwapotoshe ummma.
 
Duh arguments nyingine bwana....

Ni kweli hasimamii zote lakini ana dhamana ya barabara zote....

Ni sawa na ukiwa mkuu kazini kwako, si kazi zote unafanya na kusimamia wewe, lakini uko responsible kwa kila jambo....

Na ni wazi, ukiachilia mbali siasa, barabara nyingi ziko chini ya kiwango......kama unasafiri kwa njia ya barabara maeneo mengi utaelewa vizuri

We kweli kizibo..kama hujui mambo yanavyokwenda nenda hata kwenye vijiwe vya kahawa watakupa tofaut kati ya bararaba za manispaa na Bara ba4a zilizo chini ya TANROADS
 
Je, DC akipewa hiyo ripoti ataweza kumwajibisha waziri?

Dc anasimamia ilani ya chama akiona kuna mapungufu yapo kwa utendaji anaweza kumuwajibisha ila ni mpaka ile barabara iwe ndani ya jurisdictions zake. Barabara za manispaa hazumhusishi Waziri labda awe amesema zisimamiwe na TANROADS
 
Baada ya kuunda tume ya uchunguzi kuhusu barabara za kinondoni. Report aliyopatiwa inaonyesha madudu mengi ya uchakachuaji. Madudu ambayo yalianzia katika ngazi za utoaji tenda na mpaka ujenzi wa barabara. Mfano barabara moja ilipangwa itumia milioni 450 lakini mpaka sasa imekula 1.6bilion.

Swali?
1) Je, waziri magufuli hakuona madudu haya..?
2) Je, kama tukifuatilia barabara zingine alizojenga si mabilioni tamepotea.?
3) Kwa maana hii ripoti ya cag iliyoonyesha mabilioni kupotea ilikuwa sahihi.
4) Je, tukimpa urais ataweza kuzuia wizi wa namna hii kweli...?

Mdau unaonaje?
Bro ulikua unasemaje??..

Wadau tunaonaje??? Like seriously bro

Ama kweli hakuna anayeijua kesho yake!
 
Back
Top Bottom