“Uchaguzi huu utakuwa huru, Utakuwa na Haki”. Haya ni maneno ya Uhakikisho yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mwl. Raymond Mwangwala wakati akiongoza matembezi ya taratibu ‘Jogging’ kwa Wananchi, Watumishi wa Umma na Taasisi mbalimbali zilizopo Wilayani humo yakiwa na lengo la kuhamasisha Wananchi kujitokeza kupiga kura kuwachaguwa viongozi wa Serikali za Mitaa Novemba 27, 2024.
Matembezi hayo yamefanyika mapema asubuhi ya leo Jumatatu Novemba 25, 2024 yakiwa pia niyakuhitimisha uhamasishaji upigaji Kura zikiwa zimesalia siku mbili pekee kufikia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
DC Mwangwala pia amesema kuwa Kwenye uchaguzi huo 4R zote za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan zitatumika kikamilifu huku akiwahakikishia Wananchi kuwa watampata Kiongozi wamtakae na watakae mchagua.
Pia ameongeza kuwa ukikwepa kupiga kura na kumchagua kiongozi wa Serikali za Mitaa hautakuwa na haki yakuuliza maendeleo au kulaumu kitu chochote kwani uchaguzi huo ndio msingi wa mambo yote ya maendeleo.
“Uchaguzi huu utakuwa huru, Utakuwa na Haki”. Haya ni maneno ya Uhakikisho yaliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro Mwl. Raymond Mwangwala wakati akiongoza matembezi ya taratibu ‘Jogging’ kwa Wananchi, Watumishi wa Umma na Taasisi mbalimbali zilizopo Wilayani humo yakiwa na lengo la kuhamasisha Wananchi kujitokeza kupiga kura kuwachaguwa viongozi wa Serikali za Mitaa Novemba 27,2024.