MTANZANIA620
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 105
- 116
DC SHAKA: MSITUMIE MAJERAHA YENU KAMA BIASHARA, PELEKENI WAHALIFU MAHAKAMANI
Na Mwandishi Wetu, Kilosa - Morogoro
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mheshimiwa Shaka Hamdu Shaka, amewataka wakulima wa Kata ya Magole na maeneo jirani kuacha tabia ya kugeuza majeraha na ukatili wanaofanyiwa na wafugaji kuwa chanzo cha kujipatia fedha badala ya kutafuta haki mahakamani.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Magole, Mhe. Shaka alisema kuwa tabia ya baadhi ya wakulima kukubali kulipwa fedha na wafugaji baada ya kufanyiwa ukatili ndiyo inayochangia migogoro ya wakulima na wafugaji kutokwisha Wilayani humo.
DC Shaka amewataka wananchi hao kwa msisitizo mkubwa kushirikiana na vyombo vya dola ili kukomesha vitendo hivyo.
"Mnapofanyiwa ukatili, mnachukua pesa kwa wafugaji na kesi zinapofika mahakamani mnakataa kwenda kutoa ushahidi. Matokeo yake shauri linakosa ushahidi na mhalifu anaachiwa. Kufanya hivyo, miili yenu mnaiweka kama kitega uchumi," alisema DC Shaka kwa sauti ya msisitizo.
Aliongeza kuwa kitendo hicho cha wananchi kupokea rushwa ya kumaliza kesi nje ya mahakama kinarudisha nyuma juhudi za Serikali za kumaliza migogoro ya ardhi na kuhakikisha kunakuwepo na amani ya kudumu kati ya pande hizo mbili.
Wito kwa Vyombo vya Dola
Mhe. Shaka amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Jeshi la Polisi na uongozi wa vijiji ili watuhumiwa wote wa matukio ya ukatili wachukuliwe hatua kali za kisheria bila kujali ni mkulima au mfugaji.
Mkutano huo ulihudhuriwa na mamia ya wananchi wa Kata ya Magole, wakiwemo wazee, akina mama, vijana, pamoja na viongozi wa ulinzi na usalama wa Wilaya, ambapo wananchi walipata fursa ya kueleza kero zao.
Hatua hii inakuja ikiwa ni muendelezo wa ziara za Mkuu wa Wilaya katika kata zote zenye migogoro ya wakulima na wafugaji Wilayani Kilosa.