DC Shaka: Nitahakikisha Watendaji wote wa Serikali ambao ni wanufaika au chanzo cha migogoro baina ya wakulima na wafugaji wanachukuliwa hatua Kali

DC Shaka: Nitahakikisha Watendaji wote wa Serikali ambao ni wanufaika au chanzo cha migogoro baina ya wakulima na wafugaji wanachukuliwa hatua Kali

CM 1774858

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2021
Posts
5,621
Reaction score
5,029
IMG-20230216-WA0225.jpg

Tumejipanga na tunakuja na mkakati kabambe kumaliza Migogoro ya wakulima na wafugaji alisema Shaka,

Kwa msisitizo alisema, Nataka tuandike pamoja historia ya kumaliza kabisa changamoto ya migogoro hii Kilosa.

Namimi nikiwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya hii nitaanza na watendaji ndani ya serikali ambao ni sehemu ya ustawi au wanufaika wa migogoro hiyo alitoa angalizo Mr Shaka.

Niwahahakishie kama kuna mtu yeyote miongoni mwetu, anafaidika na migogoro hii ama anahusika kwa namna moja ama nyingine kuistawisha atakutana na mkono mkali wa sheria kwenye hili hatutangaliana usoni"

Kauli ya DC Shaka Hamdu Shaka wakati akiweka msisitizo asubuhi Alkhamis 16 Februari 2023 alipokuwa akiongea na Madiwani katika kikao cha Baraza la Halmashauri ya Wilaya Kilosa ambapo wakati wa Jioni alipata fursa kufika eneo la Magomeni ambako wananchi walifikisha malalamiko yao ofisini kwake jana.

#Kilosa2Fursa2
#Maendeleo endelevu
 
Aache utapeli, hayo mambo hayajaanza wiki iliyopita. Hapo anasaka kiki tu sio zaidi ya hapo.
Hata Mama Samia mambo anayoyafanya hayajaanza leo,hapo unasemaje!!??
 
Safi Sana Shaka,Wakupeleke Shy kuna nafasi wazi
 
Back
Top Bottom