DC Temeke: Mbagala Rangitatu kulipofanyika bomoabomoa ni eneo la wazi, tulishinda kesi na tulishatoa taarifa waondoke

DC Temeke: Mbagala Rangitatu kulipofanyika bomoabomoa ni eneo la wazi, tulishinda kesi na tulishatoa taarifa waondoke

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Baada ya kutokea kwa bomoabomoa ~ Wananchi wa Mbagala Rangitatu wadai kubomolewa makazi, vibanda vya biashara wakati kesi iko mahakamani Serikali imetoa ufafanuzi wa kilichotokea...

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda amesema:
Eneo hilo ni lwa wazi (open space), hao wanaolalamikika walivamia na tuliwapa taarifa mapema, kesi ilienda mahakamani na tukawashinda.

Tulitoa taarifa siku tatu kabla ili wahamishe vitu vyao na wapishe eneo hilo ambalo linatarajiwa kutumika kwa ajili ya matumizi ya mradi wa Stendi mpya, lakini hawakutaka kuondoka na walikuwa wanavuta muda ili wakakate rufaa na mchakato usimame.

Eneo hilo tunatarajiwa kujenga Stendi ya Mbagala kwa kuwa eneo linalotumika kwa sasa kama Stendi siyo la Serikali, ni eneo la mtu binafsi na anagawana na Serikali asilimia 50 kwa 50.

Serikali haiwezi kufanya maboresho katika eneo la mtu binafsi, kwani mwisho wake itaonekana kuna mazingira ya upigaji wa watu wa Serikali kugawana na huyo mtu binafsi.

Itambulike kuwa Serikali haiwezi kukubali au kuwaonea Wananchi wake, tulichokifanya ni sehemu ya utekelezaji wa Sheria na taarifa ilitoka mapema kama nilivyoeleza.
 
Jana nilienda chamazi ile majira ya saa mbili kasoro JIRANI na kituo cha mwendokasi kile cha kuvuka juu kwa chini niliona kundi kubwa la watu na difendar la police na maaskari wakiwa na gear zao.

Ghafla nikaona Tinga Tinga likibomoa gowdown lipo barabara Lina rangi ya blue lime chorwa safar large...

Nika pita zangu kuatuu mbele kwa mbeleeeeee
 
Kama ni open space, ilikuwaje watu wakaishi hapo kwa muda mrefu bila hatua kuchukuliwa mapema?
 
Jana nilikuwepo hapo mbagala nimeshuhudia namna watu walivyopoteza Mali zao na wengine wakizimia baada ya biashara zao kuvunjwa.
Kama ni stendi ya mabus ya mkoani mbona sehemu yenyewe ni ndogo Sana pia inakuaje hili ghorofa la tiger hotel limeachwa halijaguswa?
 
Back
Top Bottom