DC Ubungo: Hakuna Shule inauzwa Ubungo

DC Ubungo: Hakuna Shule inauzwa Ubungo

BabaMia

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2024
Posts
270
Reaction score
554
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko amekanusha taarifa zilizozua taharuki mitandaoni kwamba Shule ya Msingi ya Ubungo National Housing ambayo ni ya Serikali, imeuzwa kwa Wawekezaji.

Akiongea leo November 13,2024 kwenye mahojiano maalum na Ayo TV akiwa Shuleni hapo, DC Bomboko amesema Shule hiyo haiuzwi na wala hakuna mpango wa kuiuza.

Ameeleza zaidi kuwa upo mpango wa kuipandisha hadhi Shule hiyo kuwa English Medium hivyo amewataka Wazazi kutokuwa na hofu kwamba hata ikipandishwa hadhi Watoto wanaosoma Shuleni hapo watapewa kipaumbele na hakuna atakayehamishwa.

“Shule hii ina Watoto 600 ni Mtu Mjinga au Mpumbavu anaweza kufikiria Watoto 600 Serikali inaweza kuwatelekeza kwa kuuza Shule ambayo ni mali ya Umma au mali ya Serikali, kuna madarasa mapya manne, hatuwezi kuwa na mpango wa kuuza Shule halafu tunaendelea kujenga madarasa” ——— DC Bomboko.

Pia Soma: DOKEZO - Taharuki yazuka, Wazazi wajaa Shule ya Msingi Ubungo NHC baada ya taarifa kuwa shule inauzwa
 

Attachments

  • 1731519288457.jpg
    1731519288457.jpg
    328.5 KB · Views: 7
Aliwashirikisha Wazazi Wa Watoto Wanaosoma Hiyo shule juu ya huo Mpango Wa Kuipandisha hadhi hiyo shule..?
 
Ameeleza zaidi kuwa upo mpango wa kuipandisha hadhi Shule hiyo kuwa English Medium hivyo amewataka Wazazi kutokuwa na hofu kwamba hata ikipandishwa hadhi Watoto wanaosoma Shuleni hapo watapewa kipaumbele na hakuna atakayehamishwa
Swahili medium, yuko std 3-7, unamuhamishia english medium alafu unasema unampa kipaumbele….na hakuna atakae hamishwa,.. watatemwa na mfumo automatically,,,,,,
😂😂😂
 
Kuibadilisha shule kuwa english medium ni kuipandisha hadhi?
 
Kuibadilisha shule kuwa english medium ni kuipandisha hadhi?
Tunajizarau sana Waafrika kwa mfano kweli Kiongozi wa China au Urusi atamke kwa wananchi wao wanaipandisha hadhi shule zao kwa kuibadilisha kuwa English medium na bado akaendelea kuwa Kiongozi?
 
Back
Top Bottom