DC Ubungo: Kusema kwamba “ukristo unashambuliwa” au “Kanisa linalengwa” ni upotoshaji wa makusudi ambao sitaukalia kimya

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Kusema kwamba “ukristo unashambuliwa” au “Kanisa linalengwa” ni upotoshaji wa makusudi ambao sitaukalia kimya. Kusema waumini Milioni 3 na zaidi ya Makanisa 2,112 yamefungiwa nchi nzima sio kweli.

IMANI YA KILA MMOJA INAHESHIMIWA NA KULINDWA KWA MUJIBU WA SHERIA. Haki na Wajibu. Tarehe 20/7/2025 tulikubaliana kukutana Alhamisi tarehe 24/07/2025 saa mbili Asubuhi Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ili kuepusha mivutano isiyo na lazima. Lakini haikuwa hivyo!

Hakuna aliyefika kwa maelezo kwamba kuna kesi Mahakamani. Kama ndivyo, maana yake basi napaswa kusimamia maamuzi yaliyopo mpaka kesi imalizike Mahakamani 🤷🏿‍♂️🤷🏿‍♂️. Kutii sheria sio jambo la hiari. Kupuuza busara kwa kukosa hekima ni ukaidi wa makusudi.

Your browser is not able to display this video.
 
Msando ni jina la Kichagga lenye maana ya "mchanganyo/mchanganyiko".

Msando amewahi kuwa diwani wa Kata ya Mabogini, Moshi Vijijini na Mwanasheria Mwandamizi wa CHADEMA.
 
H
Haya ni maneno ya mkuu wa wilaya kweli au kuna mtu kumuwekea maneno mdomoni? Sitaki kuamini moja kwa moja. Vinginevyo hali ya UCHAWA Ni kubwa mno. Sijui hili tatizo litaishaje? Mungu tusaidie watz
 
Kwa hiyo ametunisha misuli?
 
Mwili wa huyo msando kama unatumikia mapenzi mema ya Mungu wa mbinguni basi ndio Kanisa lenyewe

Kanisa siyo Jengo wala taasisi 😄🙏🇮🇱
 
Kama aliyesema hayo ni DC basi imekaa poa sana
 
sidhani kama msando ni saizi ya hao jamaa. msando ni kinyangarika kidogo sana tena kisichokuwa na uhakika wa ukuu wa wilaya. waacheni waumini wamwabudu Mungu au la subirini Mungu awakate vichwa ili iwe fundisho kwa wengine. gusa vyote ila usiguse imani ya mtu, hata ningekuwa mimi nisingeenda, kwanini nijibembeleze kwa msando nikampigie goti kwa haki yangu ya kikatiba ya kuabudu? yaani msando ndio anataka awe wa kutoa fadhila? jambo la haki ya kikatiba anataka awe kama ametoa fadhila? watu wampigie magoti? aende zake huko, na washindwe kwa Jina la Yesu. cha muhimu wawe na akiba ya maneno na matendo. Mungu yupo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…