Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Tunaendelea katika episode nyingine ya Mama anaupiga mwingi na kunenepesha ng'ombe siku ya mnada!
=====
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini, Felician Mtahengerwa, ameendelea na ziara zake katika kata za Murieti, Olasiti, na Osunyai, akiwahamasisha wananchi kudumisha amani na mshikamano. Katika ziara hiyo, Mtahengerwa amewataka wananchi kukataa viongozi wanaopandikiza siasa za chuki na vurugu, akisisitiza kuwa amani ni tunu ya thamani ambayo Watanzania na wakazi wa Arusha wanapaswa kuilinda kwa nguvu zote.
“Msiingie katika siasa au mipango inayoweza kuharibu amani ya nchi yetu. Amani ni msingi wa maendeleo na ustawi wa jamii yetu,” alisema Mtahengerwa huku akitoa wito kwa wananchi kuzingatia misingi ya upendo na mshikamano kwa maendeleo ya taifa.
Ziara hizi ni muendelezo wa juhudi za mkuu huyo wa wilaya katika kuhakikisha wakazi wa Arusha wanaelewa miradi ya maendeleo iliyotekelezwa chini ya uongozi wa Rais Samia lakini pia kuwajulisha fursa zinazopatikana Arusha mjini, lakini zaidi sana ametumia ziara hizi kumsikiliza na kutatua kero za wanaanchi katika kata mbalimbali