DC Wilman Ndile: Kama kuna Wananchi hawajalipwa fidia ya kuhama Bonde la Mto Ruhila waje ofisini milango ipo wazi

DC Wilman Ndile: Kama kuna Wananchi hawajalipwa fidia ya kuhama Bonde la Mto Ruhila waje ofisini milango ipo wazi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Uongozi wa Wilaya umetoa maelezo kuhusu madai ya kuwepo kwa Wananchi ambao hawajalipwa fidia ya kuhama katika Bonde la Mto Ruhila ambapo wametakiwa kuhama ili kupisha sehemu hiyo ya hifadhi.

Mdau wa JamiiForums alidai Wananchi wanaendelea kutumia bonde hilo kwa shughuli za kibinadamu kama vile kilimo, kufua na kuoga hata baada ya kulipwa fidia na wengine hawajalipwa ndio maana wamegoma kuhama huku wakiwatishia Mgambo kwa mapanga pindi wanapoenda kutaka kuwaondoa.

Kusoma hoja ya awali, soma hapa ~ Kitendo cha Wananchi kugoma kuhama katika chanzo cha maji Bonde la Mto Ruhila na kuwafukuza Mgambo kwa Mapanga si dalili nzuri
Wilaya ya Songea Ndugu Wilman Kapenjama Ndile.jpg

Mkuu wa Wilaya ya Songea, Wilman Kapenjama Ndile
UFAFANUZI WA MKUU WA WILAYA
JamiiForums
imezungumza na Mkuu wa Wilaya ya Songea, Wilman Kapenjama Ndile ambaye anatoa maelezo kuhusu hoja hiyo:

Bonde la Mto Ruhila ni eneo ambalo maji ya Mji wa Songea yanapatikana, Serikali ilifamnya utaratibu wa kuwahamisha Wananchi waliokuwa wanaishi katika eneo hilo la Bonde kwa kuwalipa fidia.

Wananchi wamelipwa fidia katika awamu tatu, ya mwisho ilikuwa Septemba 2024 ambapo walilipwa Shilingi Milioni 900, mpaka sasa wameshalipwa wote na hakuna anayedai.

Kama wapo ambao hawajalipw awaje Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa kuwa yenyewe ndiyo ilikuwa inasimamia zoezi hilo, inawezekana kweli kuna watu wamerukwa, kazi za binadamu zinaweza kuwa na makosa na kama yap oni wajibu wetu kuyarekebisha.

Milango yetu ipo wazi, kama kuna ambaye ana changamoto ya kutolipwa afike ofisini kwetu tutamsikiliza, tutamtuma Afisa Ardhi, Afisa wa Mkuu wa Wilaya na Afisa wa Bonde la Mto Ruhila.
IMG_20241208_154934.jpg
Kuhusu Mgambo wapo chini ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ambapo hapo kuna Afisa wa Jeshi la Akiba ambaye ni Meja, ili Mgambo waende kwenye kazi lazima atumwe, pia Meja hawezi kutuma Mgambo site kama Mkuu wa Wilaya hana taarifa.

Inawezekana kuna Mgambo wamejichukulia hatua mkononi na kwenda, kama wapo wamefanya hivyo watakuwa wanakosea, mimi Mkuu wa Wilaya sina taarifa ya Mgambo kutumwa na kwamba wanaenda kutumia nguvu kuwaondoa Wananchi.
 
Back
Top Bottom