DCEA: Tuna orodha ya Wasanii wanaotumia Dawa za Kulevya, kupimwa wote

DCEA: Tuna orodha ya Wasanii wanaotumia Dawa za Kulevya, kupimwa wote

Akiongea leo November 14,2023 Jijini Dar es salaam, Lyimo amesema “Nitoe wito kwa Wasanii wanaotumia dawa za kulevya tuna orodha yao, tuna orodha ya wanaovuta bangi, tuna orodha ya wanaovuta heroin na cocaine, tunawapa muda wa kujirekebisha hii mitambo yetu ya maabara ikikamilika tutawachukulia hatua wote tutawapima na tukijiridhisha mnatumia mtachukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa Mahakamani”
Kama una orodha, sheria zipo, watendaji wapo, vifaa vipo unasimama jukwaani kufanya nini? Blabla za nini? Unamwogopa nanani na kwanini?
 
Yaani wanamfata msanii alipo wanamchukua na kumpeleka maabara?
Kwa kutumia sheria ipi naomba kueleweshwa
serikali ndio yenye mamlaka ya kila kitu hata hiyo pumzi wamekuazima tu ukiitumia vibaya wanaichukua...!

nadhani mtumiaji hana makosa mwenye makosa ni anae yaingiza hayo madawa...! wangepambana na wauzaji...ingekuwa poua sana
 
Bila kuwa na sheria hawana mamlaka yoyote.

Unamfataje mtu from no where utake kumpima? Ndicho nachotaka kufahamu
 
Back
Top Bottom