DCEA yakamata Dawa za Kulevya aina ya Heroin ambazo zingeathiri Watu milioni 4.8

DCEA yakamata Dawa za Kulevya aina ya Heroin ambazo zingeathiri Watu milioni 4.8

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo amesoma ripoti ya Operesheni iliyofanywa na mamlaka hiyo kuanzia Machi 25, 2023 hadi Juni 19, 2023 ikiwa ni takribani miezi miwili na wiki tatu ambapo amefafanua mambo mbalimbali kuhusu uhalifu wa dawa za kulevya
IMG_20230620_013210_250.jpg

Lyimo amesema katika Operesheni yao kwa mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Kilimanjaro na Arusha wamekamata watuhumiwa 109 wakiwa na dawa mbalimbali baadhi ni Heroin Kg 200.5, Heroin kete 3,878, Cocaine kete 138 ikiwemo Bangi kavu iliyotayari kisafirishwa nje gunia 978, bangi mbichi gunia gunia 5, 465, bangi iliyosindikwa (Skanka) kilo 1.5 huku ikiteketekeza eka 1093 za mashamba ya bangi.

Amesema kuwa kiasi cha Heroin kilichokamatwa kingeweza kutumiwa na kuathiri watu milioni 4.815, wakati ambapo baadhi ya watuhumiwa wamefikishwa Mahakamani wakati wowote taratibu za kisheria zitakapokamilikia.

Mamlaka hiyo imewatahadharisha Wanawake wanaojiingiza kwenye mahusiano na Wanaume raia wa kigeni ambao wamekuwa wakiwapangia nyumba na kuwahudumia bila kujua shughuli halisi wanazofanya.

Amesema baadhi ya raia hao wanaanzisha uhusiano na Wanawake zaidi ya mmoja na kuficha dawa za kulevya kwenye nyumba za wenza wao hao wakati wao wakiishi kwingine na inapotokea Wanawake hao wanapokamatwa kwa kujihusisha na biashara hiyo haramu huwakana.

“Kutokana na udhibiti kuwa mkubwa, Wafanyabiashara wa Dawa za Kulevya wameendelea kubuni mbinu mpya za usafirishaji ili kukwepa kukamatwa.

“Mamlaka imebaini mbinu hizo na kuchukua hatua, mbinu mojawapo inayotumika ni Raia wa kigeni mmoja kuanzisha mahusiano ya kimapenzi na Wanake wa Kitanzania zaidi ya mmoja na kuficha Dawa za Kulevya kwenye makazi ya Wanawake hao huku wao wakipanga nyumba tofauti na wanakoishi Wapenzi wao.

“Hali hii husababisha Wanawake wa Kitanzania kuingia kwenye matatizo makubwa ya kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria huku Wanaume wakiwakana Wanawake hao, Mamlaka imejipanga kikamilifu kupambana na biashara ya dawa za kulevya hivyo wanaojihusisha au wenye mpango wa kujihusisha na biashara hiyo waache mara moja au wajisalimishe wenyewe kabla hawajafikiwa na mkono wa sheria.

“Wananchi wanapaswa pia kuwa makini na mizigo wanayopewa kubeba au kuhifadhi pasipo kujua ndani yake kuna nini, Wanawake wanatakiwa kuwa makini zaidi kwani katika baadhi ya matukio wamekuwa wakitumiwa na Wapenzi wao hasa Raia wa kigeni kusafirisha na kupokea mizigo wasiyoijua na wakati mwingine mizigo hiyo huwa na dawa za kulevya na hivyo hujikuta matatani.”
IMG_20230620_013209_743.jpg

Amesisitiza kuwa mamlaka imejipanga kukabiliana na wanaojihusisha na biashara hiyo ya kihalifu.

MAKUBALIANO NA TAKUKURU
Ameongeza kuwa “Katika kuendelea kukabiliana na wahalifu mbalimbali tumeingia makubaliano na TAKUKURU kutumia klabu zao zilizoanzishw akwenye shule na vyuo kutoa elumu ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya.

RAIS SAMIA MGENI RASMI KATIKA MAADHIMISHO
“Mwezi Juni kila mwaka, Tanzania huungana na mataifa mengine Duniani katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupinga Dawa za Kulevya Duniani kwa lengo likiwa kuongeza uelewa wa jamii na kuhamasisha kushiriki katika mapambano dhidi ya Dawa za Kulevya Duniani.

Mwaka huu Maadhimisho hayo yatafanyika KitaifaJuni 23 hadi 25 Jijini Arusha kwenye Uwanja wa Sheik Amri Abeid yakiambatana na maonesho ya shughuli mbalimbali za udhibiti wa Dawa za Kulevya zinazofanywa na mamlaka na wadau wake na utoaji elimu wa

Mgeni rasmi siku ya kilele Juni 25, 2023 anatarajiwa kuwa Rais Samia Suluhu Hassan, kauli mbiu ikiwa ni “Tuzingatie Utu na Kuboresha Huduma za Kinga na Tiba”.
 
Barua hii imewatweza wanawake wa ki-Tanzania, ilifaa kufanyiwa proofreading kabla ya kutolewa hadharani. Ninaamini @TAMWA na TGNP wameliona hili
 
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo amesema Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama imefanya operesheni katika Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Kilimanjaro na Arusha na kufanikiwa kukamata dawa za kulevya aina ya heroin kilogramu 200.5.

Akiongea leo Dar es salaam, Lyimo amesema “Tumekamata pia bangi kavu iliyokuwa tayari kusafirishwa gunia 978, bangi mbichi gunia 5,465, bangi iliyosindikwa (skanka) kilogramu 1.5, methamphetamine gramu 531.43, heroin kete 3,878, cocaine kete 138, mililita 3,840 za dawa tiba zenye asili ya kulevya aina ya Pethidine pamoja na kuteketeza ekari 1,093 za mashamba ya bangi”

“Aidha, kwa kushirikiana na Bodi ya Kimataifa ya Kudhibiti Dawa za Kulevya (INCB) Mamlaka imezuia kuingia nchini jumla ya kilogramu 1,507.46 za kemikali bashirifu ambazo zingeweza kutumika kutengenezea dawa za kulevya”

“Ukamataji huo uliofanyika kuanzia tarehe 25 Machi, 2023 hadi tarehe 19 Juni, 2023 unahusisha Watumiaji 109 wakiwemo Raia watatu wa kigeni, baadhi ya Watuhumiwa wamefikishwa Mahakamani na wengine wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani taratibu za kisheria zitakapokamilika”
 
... bila shaka motivational speakers wanaoanza na biashara ya kuuza ubuyu pesa kwenye kibubu! Wanawashangaa vijana na degree zenu mnahangaika mtaani badala ya kujiajiri!
 
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Aretas Lyimo amesema Mamlaka hiyo kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama imefanya operesheni katika Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Kilimanjaro na Arusha na kufanikiwa kukamata dawa za kulevya aina ya heroin kilogramu 200.5.

Akiongea leo Dar es salaam, Lyimo amesema “Tumekamata pia bangi kavu iliyokuwa tayari kusafirishwa gunia 978, bangi mbichi gunia 5,465, bangi iliyosindikwa (skanka) kilogramu 1.5, methamphetamine gramu 531.43, heroin kete 3,878, cocaine kete 138, mililita 3,840 za dawa tiba zenye asili ya kulevya aina ya Pethidine pamoja na kuteketeza ekari 1,093 za mashamba ya bangi”

“Aidha, kwa kushirikiana na Bodi ya Kimataifa ya Kudhibiti Dawa za Kulevya (INCB) Mamlaka imezuia kuingia nchini jumla ya kilogramu 1,507.46 za kemikali bashirifu ambazo zingeweza kutumika kutengenezea dawa za kulevya”

“Ukamataji huo uliofanyika kuanzia tarehe 25 Machi, 2023 hadi tarehe 19 Juni, 2023 unahusisha Watumiaji 109 wakiwemo Raia watatu wa kigeni, baadhi ya Watuhumiwa wamefikishwa Mahakamani na wengine wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani taratibu za kisheria zitakapokamilika”

Jina tu linamtambua ni mchagga, aswekwe ndani haraka na iwe fundisho kwa wengine
 
... ila hili la bhange ni la kuangalia upya. Hii kitu ihalalishwe tu maana ni kama jamii inataka hivyo.
 
Back
Top Bottom