LAZIMA NISEME
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 262
- 297
Mwezi Machi na Aprili, 2025 Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwakushirikiana na vyombo vingine vya dola imefanya operesheni Katika mikoa ya Dar es Salaam,shinyanga, Tabora, Tanga, Songwe, Mbeya na Arusha na kufanikiwa kuzuia tani 14 za kemikalibashirifu zilizokuwa ziingizwe nchini kinyume cha sheria, kukamata pakti 10 za pipi zenye uzito wagramu 174.77 zilizotengenezwa kwa kutumia bangi, kukamata kilogramu 4,568 za dawa mbalimbali zakulevya, kuteketeza ekari 178 za mashamba ya bangi pamoja na kushikilia magari saba, pikipiki tanona bajaji moja vilivyohusika kwenye uhalifu huo. Jumla ya watuhumiwa 35 wamekatwa na taratibu zakisheria zinaendelea dhidi yao.
Kwa kushirikiana na Bodi ya Kimataifa ya Kudhibiti Dawa za Kulevya Duniani (INCB) na mamlakanyingine za udhibiti, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ilibaini na kuzuiakilogramu 4,000 za kemikali aina ya 1-Boc-4-piperidone na kilogramu 10,000 za kemikali aina yaAcetic anhydride zilizokuwa ziingizwe nchini kutokea bara la Asia bila kuwa na vielelezovinavyoonesha matumizi ya kemikali hizo. Endapo kemikali hizi zingeingizwa nchini na kuchepushwazingeweza kutumika kutengeneza dawa za kulevya aina ya fentanyl na heroin.
Mathalani, kilogramu 4,000 za kemikali aina ya 1-Boc-4-piperidone zinaweza kutengeneza kilogramu8,000 za dawa za kulevya aina ya fentanyl. Matumizi ya kiasi hicho cha dawa za fentanyl ambazozingezalishwa zingeweza kusababisha vifo kwa watumiaji bilioni nne (4) ikizingatiwa kwamba,kilogramu moja (1) ya dawa hizo inaweza kusababisha vifo kwa watu 500,000 kutegemea na uzito, afya, na historia ya mtumiaji (miligramu mbili (2) inaweza kusababisha kifo kwa mtu mmoja).
Kemikali aina ya acetic anhydride inaweza kutumika katika mchakato wa kutengeneza dawa zakulevya aina ya heroin. Hivyo, kiasi cha kilogramu 10,000 kilichozuiliwa kingeweza kutumikakutengeneza kilogramu 3,704 za heroin. Aidha, kemikali hiyo inaweza kutumika kuzalisha kemikalinyingine bashirifu ambazo zinaweza kutumika kuzalisha dawa za kulevya za mandrax namethamphetamine. Uchunguzi wa kina kwa kushirikiana na taasisi za kimataifa unaendelea ili kubainimitandao zaidi ya usafirishaji haramu wa kemikali bashirifu zinazoweza kuchepushwa na kutengenezadawa za kulevya.
Katika operesheni zilizofanyika mkoani Mbeya, raia wa Uganda Herbert Kawalya mwenye hati yakusafiria Na. B00132399 na mmiliki wa kampuni ya Hoxx Wells Lux Tour Limo, alikamatwa akiwa napakti 10 za pipi zenye uzito wa gramu 174.77 zilizotengenezwa kwa dawa za kulevya aina ya bangiyenye kiwango kikubwa cha sumu ya tetrahydrocannabinol (THC).Ukamataji huo, ulikwendasambamba na ukamataji wa gari ndogo aina ya Mercedes Benz yenye namba za usajili MG 33 BM GPiliyokuwa inasafirisha pipi hizo kuingia nchini kutokea Afrika Kusini. Utengeneza wa pipi hizi zenyekiwango kikubwa cha sumu aina ya THC ni ushahidi wa nia ovu ya wahalifu kulenga kuharibu vijanaambao ndio nguvu kazi ya Taifa.
Aidha, katika tukio lingine mkoani Mbeya, zilikamatwa kilogramu 1,658 za bangi aina ya skanka nakilogramu 128.7 za bangi zilizokuwa zinaingizwa nchini kutoka nchini Malawi.
Operesheni zilizofanyika Jiji Dar es Salaam, zilifanikisha ukamataji wa kilogramu 220.67 za bangi aina
ya skanka katika kata ya Chanika zikiwa zimefichwa chooni huku kilogramu 11 zikikamatwa eneo laukaguzi wa mizigo kwenye bandari ya kuelekea Zanzibar.
Katika operesheni zilizofanyika mikoa ya Arusha, Tanga, na Manyara zilikamatwa kilogramu 733.74 zadawa ya kulevya aina ya methamphetamine, kilogramu 91.62 za heroin, kilogramu 692.84 za mirungiiliyokuwa inaingizwa kutokea nchini Kenya na kilogramu 115.05 za bangi pamoja na kuteketeza ekarimbili (2) za mashamba ya bangi. Vilevile, operesheni zilizofanyika katika Wilaya ya Uyui na Nzegamkoani Tabora, kilogramu 845 za bangi zilikamatwa na ekari 176 za mashamba ya bangiziliteketezwa. Kadhalika, kilogramu 98.35 za dawa za kulevya aina ya bangi zilikamatwa katikaoperesheni zilizofanyika wilayani Kahama na Shinyanga.
Udhibiti wa dawa za kulevya na kemikali bashirifu uliofanyika, umezuia athari kubwa ambazozingejitokeza kiafya, kijamii, kiuchumi na kimazingira ikiwemo kuongezeka kwa dawa za kulevyamtaani. Pia, ukamataji huu umesaidia kuokoa nguvu kazi ya Taifa ambayo ingeangamia endapo dawahizo zingeingizwa mitaani.
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) inatoa wito kwa wananchikuendeleza ushirikiano kwa kutoa taarifa mapema wanapohisi au kuona uwepo wa shughulizinazohusiana na biashara au uzalishaji wa dawa za kulevya katika maeneo yao kupitia kituo chetu chataarifa na huduma kwa kupiga namba 119 bure. Vilevile, wazazi na walezi mnahimizwa kuwa makinina kufuatilia kwa karibu mienendo ya watoto wenu ikiwa ni pamoja na kuwaasa wajiepushe namazingira na sababu zozote zinazoweza kuwaingiza kwenye matumizi ya dawa za kulevya.
Pia, tunazikukumbusha kampuni zinazojihusisha na biashara na matumizi ya kemikali za viwandani na
kilimo kuzingatia matakwa ya sheria za nchi na kuepuka kushirikiana na magenge ya kihalifukusafirisha kemikali bashirifu ambazo zinaweza kuchepushwa na kutengeneza dawa za kulevya.