DCEA yamnasa Kinara wa Mirungi, yateketeza Ekari 285.5 Same

Huyo mama Dangote alikuwa hivyo pia serikali ikikuchoka ndio tatizo.

Huyo jamaa bado serikali haijamchoka Ila soon utasikia kitu. Huyu Lymo ni masta kabisa
 
Mama Dangote kagoma kupigwa PICHA?
KAZI ni kipimo cha utu
 
Kuchomeana ni wivu uchawi na umasikini...
CCM wanaiba mabilioni..
 
Carbon emissions project na Uharibifu wa Mazingira......Tree for Livelihoods!++
 
Too late kwao, but mwaka jana serikal ilimwaganwale vijana wake upande huo. Kulikuwa na joint operation ya taasis nyingi, nadhani ndio hii, naambiwa wale wanao kaa maeneo hayo, wale vijana wqsafirishaj mihadarati wamedimika sana siku izi
Mitaa yote ya Same mpaka Makanya na Kihurio ndio biashara yao kubwa.. Na vijana wanakula yamini ya kutochomeana.. Anayekiuka yamini humkuta ya kumkuta
 
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola, imefanya operesheni maalum wilayani Same, mkoani Kilimanjaro kuanzia tarehe 19 hadi 25 Machi 2025.

Katika operesheni hiyo, ekari 285.5 za mashamba ya mirungi zimeteketezwa na watuhumiwa saba (7) wamekamatwa, akiwemo kinara wa biashara haramu ya mirungi nchini aliyekuwa akitafutwa kwa muda mrefu, Interindwa Zinywangwa Kirumbi, maarufu kwa jina la mama Dangote.

Akizungumza baada ya operesheni hiyo, Kamishna Jenerali wa DCEA Aretas Lyimo, amesema kuwa, mama Dangote ni mzalishaji na msambazaji mkubwa wa dawa za kulevya aina ya mirungi nchini. Kwa zaidi ya miaka 30, amekuwa akiendesha mitandao ya biashara haramu ya mirungi na kusimamia masoko ya dawa hizo za kulevya katika maeneo mbalimbali nchini, licha ya kujua kuwa ni kinyume cha sheria.

Aidha, kamishna Lyimo ameongeza kuwa, mwaka juzi Mamlaka ilifanya operesheni wilayani humo na kutoa elimu kwa wananchi ili waachane na kilimo cha mirungi na badala yake wajikite katika kilimo cha mazao mbadala pamoja na ufugaji.

“Mwaka juzi tuliteketeza jumla ya ekari 535 za mashamba ya mirungi. Kwa kushirikiana na uongozi wa wilaya, tulitoa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya dawa za kulevya, ikiwemo mirungi. Lengo lilikuwa kuwawezesha wakazi wa eneo hili kujikita katika kilimo cha mazao mbadala na ufugaji kama njia ya kujiongezea kipato” alisema Kamishna Jenerali Lyimo.

Pia, Kamishna Lyimo alieleza kuwa, pamoja na jitihada hizo, uongozi wa wilaya ya Same na Wizara ya Kilimo na mifugo waliwapelekea wananchi wa maeneo hayo miradi ya ufugaji wa nguruwe na kugawa miche ya kahawa, iliki na mazao mengine.

Kutokana na juhudi hizo, wananchi wengi wameachana na kilimo na mirungi na kuanza kulima mazao mbadala, japo wapo wananchi wachache waliokaidi na kuendelea na kilimo na biashara ya mirungi.
Kamishna Lyimo amesisitiza kwamba Mamlaka itaendelea kufanya operesheni kuhakikisha wananchi wote wanaojihusisha na biashara ya mirungi wanakamatwa na hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi yao.
 
Hilo jimama lina roho ngumu, limeuza mirungi kwa muda mrefu bila kukamatwa. Huenda hata bangi limeuza sana tu. Kuna wanawake wana roho ngumu aisee, wengine huuza gongo na biashara zingine haramu na misheni za kiharamia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…