DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,153
Msemaji wa Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi DCP David Misime ametoa wito kwa Watanzania kuwa watulivu na kuepuka kuchochea vurugu au fujo siku ya kupiga kura, Oktoba 29. Ametoa tahadhari kwa wote wanaopanga kuvuruga amani, akisisitiza kuwa hata kama mgombea wako hajashinda, ni muhimu kuheshimu maamuzi ya wananchi kupitia sanduku la kura.