Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, DCP David Misime amesema kuwa Jeshi la Polisi litashirikiana na polisi jamii kubaini viashiria vyovyote vya uhalifu na vyanzo vya kuvuruga amani wakati wa kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa 2025 ili kuweza kuchukua hatua za kisheria kwa wale watakaovuruga amani.
DCP Misime ameeleza hayo tarehe 21 Agosti, 2025 katika Mkutano wa Wadau wa Sekta ya Habari na Utangazaji Kanda ya Mashariki ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) kwa kushirikiana na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo uliofanyika katika Ukumbi wa PSSF jijini Dar es Salaam ili kuhakikisha uwasilishwaji wa habari unazingatia weledi, kanuni na maadili ya kitaaluma kuelekea Uchaguzi Mkuu.
"Naomba mfahamu nilivyosema kwamba tunatumia polisi jamii siyo kwamba tunawaanda wao kusimamia mambo ya uchaguzi, wao tunataka tushirikiane na jamii tushirikiane katika kubaini uhalifu, kuzuia watu wanaopanga vitendo labda vya kuvuruga uchaguzi, kufanya fujo kwenye mikutano ya watu, ndiyo kazi tunayofanya”, amesema Misime.
Wanataka kuteka watu kwa kisingizio cha taarifa za kiintelijensia tena taarifa zilizotolewa na layman kwa sababu ya chuki za kisiasa, mapenzi na migogoro ya ardhi asee