DCs wapanguliwa na kustaafishwa

DCs wapanguliwa na kustaafishwa

Mnali je??ukute nae amehamishwa tu...maana ana back up kubwa ya wazalendo wenzake hahahh ....heri ngulume apumzike maana duu nashangaa hata hapo alipofika...mpika chai wa uwt leo mkuu wa wilayaa hahaha sio karne hii....


...Huyu mama kweli ilikuwa hamna kitu, bora amepumzishwa! seriously, aliwahi kuwa mpika chai wa UWT??
 
Wakuu,

Hivi nini maana ya kustaafishwa? Si waseme tu nani wamefukuzwa, nani wameacha kwa mapenzi yao na nani wamestaafu shauri ya umri?

Hili neno kustaafishwa linaficha madhambi mengi sana.
 
Wakuu,

Hivi nini maana ya kustaafishwa? Si waseme tu nani wamefukuzwa, nani wameacha kwa mapenzi yao na nani wamestaafu shauri ya umri?

Hili neno kustaafishwa linaficha madhambi mengi sana.
Mkuu mtanzania,
Tupo Ukurasa mmoja!nchi yetu ndiyo ipo hivi..wote wachafu so huwa wanapumzishana kwa Amani!

2010 inakuja
 
Wakuu,

Hivi nini maana ya kustaafishwa? Si waseme tu nani wamefukuzwa, nani wameacha kwa mapenzi yao na nani wamestaafu shauri ya umri?

Hili neno kustaafishwa linaficha madhambi mengi sana.

Kaka Mtanzania kuna utofauti Mkubwa kati ya "Kustaafishwa" na "kufukuzwa".Mara nyingi ukistaafishwa unalipwa marupurupu yako,lakini ukifukuzwa haki zako zinapotea.

Mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya yamekuwa ya kustusha,kwa sababu hakuna Mkuu wa Wilaya yeyote aliyepata tetesi ya kwamba mabadiliko yatakuwa lini,Kuna Dc mmoja ambaye amestaafishwa hakujua mpaka Jumanne walipoitwa Dar,hata hivyo bado kuna Wateuliwa wengi hawajapata barua rasmi za Uteuzi wao,na wamesikia habari hizi kwenye vyombo vya habari!
 
Jamaa anaandaa watu watakaomsaidia kurudi madarakani 2010
 
Hakuna jipya ,lazima CCM iondoke madarakani haya mambu ya kupokezana vijiti yamepitwa na wakati ,yaani jamaa utafikiri anacheza drafti au chess.
 
Kwa wilaya zilizopo mipakani nadhani kwa sababu za kuisalama na sometimes kuibabe,inabidi apewe mwanajeshi (hili nililishuhudia wilaya za Kigoma na kagera)

Basi kwa maana hiyo Bw. Frank Luhahula amekuwa akipewa kazi nzito, katolewa Karagwe mpakani kupambana na ng`ombe wa Uganda na majambazi wa Burundi sasa anakwenda Tarime kupambana na wakulima wa bangi na mapigano ya koo
 
Halafu 'mnasema' eti viongozi wetu ni reflection yetu wenyewe!....Please exclude me on that.
 
...Huyu mama kweli ilikuwa hamna kitu, bora amepumzishwa! seriously, aliwahi kuwa mpika chai wa UWT??
Yes ni kweli kabisa mimi sina ugomvi nae ila ndiko alikoanziaa wajua ukikaa karibu na ua ridi utanukia tu...alikuwa mpika chai makao makuu uwt anagombea mwenyekiti tawi uwt la makao makuu....akawa na mkakati wa kuzaa na wazee wa chama na kuwa kiburudisho chao...hadi akawa mwenzao....ndio maana wanamuonea huruma....ni darasa la sabala upe ngumbalu kabisa....ni ukweli kabisaa sijaongeza neno hapo hahha pia akaolewa na best wa JK anaitwa mzee(babu)Mbagulwa hahha akaolewa naeyaaani maajabu yhy ni babu yake kabisa na mzee alikuwa hoi hoi kabisaa mama akiwa mkuu wilaya bagamoyo akaolewa.....sasa. Sikiaa mahari na gharama ya harusi alitoa JK sababu ya swahiba wake hana kitu nasikia alimuuliza unaoa au unaolewa??huku akijua kuwamama hawa anajua analofanya.......true story
 
Francis Isaac (Mbulu, Manyara),

Baada ya kuiba UVCCM sasa amepewa rungu akafisadi Mbulu! jamani nchi ya kulindana hii!
 
...Yuko wapi Betty Mkwasa? naona wilaya yake ya Korogwe kapewa mtu mwingine! Fatuma Mwassa ni huyu ambaye mpaka juzi juzi ni muandishi wa habari sijui wa Majira ama kule kwa Mafisadi?? Tujuzeni....

Elizabeth Mkwasa kahamishiwa BAHI - Dodoma karibu na Ikulu ya Chamwino!!
 
Kaka Mtanzania kuna utofauti Mkubwa kati ya "Kustaafishwa" na "kufukuzwa".Mara nyingi ukistaafishwa unalipwa marupurupu yako,lakini ukifukuzwa haki zako zinapotea.

Mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya yamekuwa ya kustusha,kwa sababu hakuna Mkuu wa Wilaya yeyote aliyepata tetesi ya kwamba mabadiliko yatakuwa lini,Kuna Dc mmoja ambaye amestaafishwa hakujua mpaka Jumanne walipoitwa Dar,hata hivyo bado kuna Wateuliwa wengi hawajapata barua rasmi za Uteuzi wao,na wamesikia habari hizi kwenye vyombo vya habari!

Asante mkuu Mwawado kwa ufafanuzi.

Hivi nani anaenda kuwa DC wa Kyela?
 
Elizabeth Mkwasa kahamishiwa BAHI - Dodoma karibu na Ikulu ya Chamwino!!

Out of curiosity .... Chamwino ni Ikulu ndogo ya JK, kwa hiyo ndo kusema Elizabeth Mkwasa ni nanihiino ndogo ya Ikulu?
 
Out of curiosity .... Chamwino ni Ikulu ndogo ya JK, kwa hiyo ndo kusema Elizabeth Mkwasa ni nanihiino ndogo ya Ikulu?

Mkuu Keil,

Umeniwahi, nilitaka kuuliza swali hilo hilo, anyway tuache tusije tukaambiwa tunadhalilisha dada zetu.
 
Waliokuwa wanataka Orodha Kamili, iko hapa.

Rais Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya wakuu wa wilaya kwa kuteua wapya 15, kustaafisha saba na kuwabadilisha vituo 54. Taarifa iliyotolewa jana na Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), ilionyesha pia kuwa wakuu wa wilaya wawili watapangiwa kazi nyingine na wengine wawili wameondolewa baada ya hivi karibuni kuteuliwa kuongoza Jumuiya za Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mabadiliko haya yanatarajiwa kuongeza chachu katika usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli za maendeleo ili kuiwezesha Serikali kufikia malengo yake.

Wakuu wapya na wilaya zao kwenye mabano ni Mercy Silla (Arumeru), Norman Sigalla (Hai), Kanali Issa Njiku (Misenyi), Angelina Mabula (Karagwe), Dk. Rehema Nchimbi (Newala), Francis Isaac (Mbulu), Luteni Kanali Benedict Kitenga (Rorya) na Luteni Kanali Cosmas Kayombo (Mbarali). Wengine ni Christopher Kangoye (Kwimba), Queen Mlozi (Ukerewe), Fatuma Mwassa (Mvomero), Fatma Ally (Nanyumbu), Juma Madaha (Tunduru), Anatory Choya (Kishapu) na Erasto Sima (Korogwe).

Waliostaafishwa ni Elias Maarugu (Misenyi), Deusdedit Mtambalike (Muleba), David Holela (Babati), Hawa Ngulume (Mbarali), Mashimba Mashimba (Kyela), Kanali Peter Madaha (Nyamagana) na Gilbert Dololo (Kibaha). Wanaosubiri kupangiwa kazi nyingine ni Patrick Tsere (Ilala) na Doreen Kisamo (Uyui). Martin Shigela aliyekuwa Lindi aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM wakati Husna Mwilima aliyekuwa Hai, aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT).

Wakuu wa wilaya waliobadilishwa vituo vya kazi ni wafuatao: Elias Lali (kutoka Arumeru kwenda Ngorongoro), Evans Balama (Arusha kwenda Ilala), Jowiko Kasunga (Ngorongoro kwenda Monduli), Kanali Fabian Massawe (Kinondoni kwenda Muleba), Abdallah Kihato (Temeke kwenda Kyela) na Zainab Kwikwega (Bahi kwenda Kasulu).

Wengine ni Dk. Ian Langiboli (Chamwino kwenda Babati), Kapteni Seif Mpembenwe (Kondoa kwenda Handeni), Halima Dendego (Mpwapwa kwenda Kilosa), Lephy Gembe (Makete kwenda Chamwino), Elaston Mbwilo (Iringa kwenda Mtwara) na Darry Rwegasira (Njombe kwenda Mpwapwa). Waliohamishwa wengine ni Said Mkumbo (Chato kwenda Temeke), Frank Uhahula (Karagwe kwenda Tarime), Luteni Kanali John Mzurikwao (Kibondo kwenda Mpanda), Saidi Bwanamdogo (Kasulu kwenda Kondoa), Raymond Mushi (Rombo kwenda Arusha) na Jordan Rugimbana (Mwanga kwenda Kinondoni).

Wakuu wa wilaya wengine waliohamishwa vituo ni Rashid Ndaile (Nachingwea kwenda Chunya), Anna Magowa (Liwale kwenda Hanang), Elias Goroi (Mbulu kwenda Nachingwea), Kapteni Geoffrey Ngatuni (Hanang kwenda Musoma), Saveli Maketta (Musoma kwenda Namtumbo) na Stanley Kolimba (Tarime kwenda Uyui).

Wengine ni Miriam Lugaila (Rungwe kwenda Misungwi), Halima Kihemba (Mbozi kwenda Kibaha), Fatuma Kimario (Chunya kwenda Igunga), Athuman Mdoe (Kilosa kwenda Mwanga), Hawa Ng’humbi (Mvomero kwenda Makete), Gishuli Charles (Mtwara kwenda Njombe) na Jackson Msome (Newala kwenda Rungwe). Wengine waliohamishwa ni Kapteni Assary Msangi(Nanyumbu kwenda Iringa), Samwel Kamote (Ilemela kwenda Bukoba), Danhi Makanga (Kwimba kwenda Kibondo), Magalula Magalula (Misungwi kwenda Lindi), Paul Chiwile (Ukerewe kwenda Liwale) na Mathew Nasei (Magu kwenda Muheza).

Wakuu wengine waliohamishwa ni Luteni Kanali Serenge Mrengo (Bagamoyo kwenda Ilemela), Ali Rufunga (Rufiji kwenda Manyoni), Meja Bahati Matala (Sumbawanga kwenda Kahama), Thobias Mazanzala (Mpanda kwenda Sumbawanga) na Gabriel Kimolo (Namtumbo kwenda Mbozi). Pia wengine ni Peter Kiroya (Tunduru kwenda Rombo), Amina Masenza (Mbinga kwenda Shinyanga), Khadija Nyembo (Kishapu kwenda Chato), Kanali mstaafu Edmund Mjengwa (Shinyanga kwenda Mbinga) na Magesa Mulongo (Bukombe kwenda Bagamoyo).

Wengine ni Florence Horombe (Singida kwenda Bukombe), Pascal Mabiti (Manyoni kwenda Singida), Cleophas Rugarabamu (Igunga kwenda Nyamagana), Kassim Majaliwa (Urambo kwenda Rufiji), Luteni Winfrid Ligubi (Handeni kwenda Urambo), Elizabeth Mkwasa (Korogwe kwenda Bahi) na Zainab Kondo (Muheza kwenda Magu).

Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Kikwete kufanya mabadiliko makubwa ya wakuu wa wilaya tangu alipoingia madarakani mwaka 2005.

Source: HabariLeo
 
Mashimba hakustahili kustaafishwa bali kufukuzwa. Akiwa DC pale Kyela katika mengi alofanya ni pamoja na;
1. Kwa kushirikia na RC Mbeya wamefukarisha kina mama wauza mchele kwa kuzuia harambee yao huku wakiwa wametumia zaidi ya shilingi milioni mbili kuiandaa, kisa mgeni rasmi Prof Mwandosya.

2. Kuwahadaa wafanyakazi wa Kiwira Coal Mine kwamba anashughulikia matatizo yao kumbe anatayarisha mazingira ya rushwa, alizawadiwa VX kwa laki sita

3. Kukosa adabu mbele ya Mkuu wa Kaya alipokuwa ziarani katika Mkoa wa Mbeya mwaka jana. Alifanya utani kwa kupokea simu wakati anamsomea Rais taarifa ya wilaya na kusema "Hujui kuwa niko na bosi wangu, Mweshimiwa watu wengine bwana!" Alirudia mara mbili kitendo hicho, bw mkubwa aliishia kucheka!

4. Alifumaniwa na mkewe akiwa na hawara nyumbani kwake (DC) habari zikazaaga mji wote wa Kyela kwani haikuwa siri na walifika hadi kituo cha p[olisi kusuluhisha.

Ni wazi kwa matukio hayo amevumiliwa sana. Hivi sasa katika Mji wa Kyela watu wanasheherekea.

Kwa kweli ma DC wa KJ wanazua maswali mengi
 
- Wakuu hivi kweli tunahitaji Wakuu wa wilaya Tanzania?

FMES!

Now you are talking. Ni ulaji na wizi mtupu. Kazi zao zinaweza na zinafanywa na wakurugenzi wa halmashauri za wilaya. same thing applies for wakuu wa mikoa. Lakini ni lazima wakulu waweke vijitawi vyao (puppets) ili waweze kimarisha nguvu zao. Sioni mantiki yeyote mtu kama Kitila Mkumbo asipate
hata ukuu wa wilaya. OOps nilisahau kuwa siyo mwenzao
 
Back
Top Bottom