Tatizo ninyi wakenya uwezo wenu wa kufikiria ni mdogo sana, inafikia wakati tunachoka kujibizana na ninyi, ni sawa na mtoto mdogo anashika kidole chako na anakuuliza, " eti baba hiki ni nini?".
Kabla hujauliza swali ulipaswa ujiridhisha na kufahamu nini hicho inachouliza, sasa kama hata hujui chochote kuhusu jambo lenyewe, unawezaje kuuliza maswali ya kitoto kiasi hicho?.
Kama utafuatilia katika mitandao hili jambo limeelezwa kwa undani sana kitu gani kilitokea, ninyi kwa uwezo wenu mdogo wa akili mlionao, mnataka kutuingiza katika mjadala wa kitoto usiokuwa na maana yoyote. Hivi ni mtu gani mwenye akili timamu anayeweza kufikiria kwamba shirika la ndege linaloanzisha "new route" linaweza kufukuzwa?, acheni utoto huo.