Deadline yangu mwakani, ndoa lazima nifunge

1.
6.
Namshukuru Manani, himeni yangu salama,
Hadi huko mwakani, haitotiwa alama,
Wala siweki sokoni, yake wangu kujinoma,
Dedilaini mwakani, ndoa lazima nifunge

Malenga ninawaita, hima nisaidieni,
Nimeupata utata, kuifahamu himeni,:coffee:
Nakaribia kudata, japo ni wa kiumeni,
Nawasihi mnijuze, himeni ni kitu gani?

Miss ninakupongeza, kwa kweka hadharani,
Ndoa umeitangaza, umechoka upwekeni,
Ila umenishangaza, umeitaja himeni!:shock:
Nawasihi mnijuze, himeni ni kitu gani,


Mnijuze sifa zake, hadi mtu ajinome,
Kama dau niliweke, ili nami nijinome,
Sokoni nijipeleke, madukani nijitome,
Nawasihi mnijuze, himeni ni kitu gani?

Nakuita Klorokwini, waifahamu himeni?
Butege na Sipirini, mewahi kuioneni?
Maguluma na Amani, tafadhali nijuzeni,
Nawasihi mnijuze, imeni ni kitu gani?

Na Kaizer K. Kaizer
 

ngoja waje wajuzi, himeni watakujuza,
mie labda wa juzi, kwa mengi ninawakwaza,
hata na wewe mzazi, washindwa japo kuwaza,
himeni i kama vazi, chanwapo hiyo huliza,

umewaita malenga, kwa dogo hilo jawabu,
ungeuliza wakunga, wasingeipata tabu,
hao wako wadunga, japo wengine vibabu
himeni i kama vazi, chanwapo hiyo huliza,

washituka kujinoma, hali wajua vitamu,
wataka iwepo noma, japo ile maalumu,
kimoja hiyo hukoma, ndipo yasemwa nitamu,
himeni i kama vazi, chanwapo hiyo huliza,
 

sasa nimekufahamu, kushukuru sina budi
maneno yako matamu, yanukia kama udi
mrembo mwenye nidhamu, tena huna ukaidi
nakuombea kwa mola, wepesi akufanyie

mimi siwezi gombea, ninae wangu pembeni
lakini ninatambua, atokupata kawini
katika hii dunia , zimeadimika himeni
nakuombea kwa mola, wepesi akufanyie

mengi umeyasema , ya msingi na maana
lakini pia tazama , tabia muhimu sana
usije potea zama, mitego ni mingi sana
nakuombea kwa mola,wepesi akufanyie

mwema hutoka mbinguni,wahenga wanatwambia
usali kwa yako dini , miezi iliobakia
umpate mwandani , asije kubadilikia
nakuombea kwa mola, wepesi akufanyie

kaditamati wa tama, beti zimeniishia
nadhani niliyosema, akilini yanaingia
kama pumba nimetema, msamaha nipatia
nakuombea kwa mola, wepesi akufanyie
 
All the best my dear Judith,Blessings!:coffee:
 

sikuwa nikilijua, neno hili "himeni"
lakini nilikisia , ni neno la kizamani
yangu intelijensia, ikasema ni "ukeni"
nadhani sikukosea, kuread between ze laini.

kamanda unanitisha, na hili lako suali
ndoa umeikatisha , ulipoliona zali
himeni mekudatisha, wataka piga kabali
meza unaihamisha, mchana wa jua kali

himeni imenadiwa, kwa wenye nia thabiti
ndio maana najitowa, hii si yetu bahati
usijechanganyikiwa, kwa la jirani kabati
hii si yetu ngekewa, wala ya "babu matiti"

miss amefafanua , wengi tumenufaika
himeni tumeijua , sote tulighilibika
macho tumeyakodoa, sote sasa twaitaka
hili kweli ni balaa , vidume twasononeka

acha niishie hapa, chaki imeshamaliza
kwa alietoka kapa,ni vyema akapuuza
acha nilichape lapa, kichwa nisije umiza
aspirin kasepa , hana cha kujieleza.
 

klorokwini wanikuna, shairi ulonimbia,
hiyana kwako hakuna, dua umeniombea,
kumbe si dawa ya homa, bali ya raha kutia,
ya kwako yamenichoma, yote nitazingatia,

hata mie naombea,aliye mwema nipate,
sana mesubiria, sasa kiu nikate,
watoto nakimbilia, kwa raha niwapakate,
ya kwako yamenichoma, yote nitazingatia,

najua ipo mitego, yanasa hata vigori,
yang'oa hata magego, yachoma kama mbigiri,
mie taipa kisogo, japo sinacho kiburi,
ya kwako yamenichoma, yote nitazingatia,

Mungu nimemtumai, anipe raha milele,
ndoa nisijekinai, kama wazazi wa kale,
nisijetenda jinai, kiburi kuweka mbele
ya kwako yamenichoma, yote nitazingatia,

usia wako mwanana, lako neno maridhawa,
umeuleta kwa vina, hekima bure wagawa,
mie naupaka hina, kiwe cha wengi kipawa,
ya kwako yamenichoma, yote nitazingatia,
 
Hongera mrembo wangu Miss Judith,
Big Up sana Ndugu yangu wa Ukweli Kaizer,
Ma hommies tablets Asprini and Chlorokwini
Sababu nyingine ya kwenda counter ya juu kutafakari haya mashairi...!!
 
all the best Miss Judith hapo mwakani bila shaka mambo yatakuendea vizuri.
 
katika kutafuta, umakini wahitajika
usije ingie chaka, ukazoa takataka
ndoa ikachakachuka, na kilio kukutoka
Nakutakia lakheri, Katika yako mipango

angalizo ni busara, kwa mme mtarajiwa
roho ndio hasara, pesa ni majaliwa
Staha na furaha, ndio muhimu kupewa
Nakutakia lakheri, Katika yako mipango
 

shairi uloandika , limenipa tabasamu
tena nimefurahika, ewe ulo mkarimu
daima utasifika , kwa yako tele nidhamu
uwe wake malaika, awe wako hensamu

mengi ulioandika, yamenigusa moyoni
sifa zisizo mipaka, umenipa klorokwini
na hina ukazipaka,nashukuru kwa kunithamini
nimepokea hakika, hizo zako shukrani

natamani ningekesha, shairi kukutungia
jinsi ulivyonikosha , nashindwa kuongezea
hofu nisije chemsha, yana tabu mazowea
vina vyako vyanitisha, hakika vimetulia

hiyo siku ikifika, twaomba kuhudhuria
kama utatualika, mpunga kuja jilia
Mungu alietukuka, akupe njema afia
ufurahi na kuruka, chumbani ukiingia.
 
:sick:Hongera sana Judith! Kila la kheri kama utafanikiwa kupata mume wakweli!:A S thumbs_down:
 
Miss Judith, mashairi yako yamesimama, Big up kwa sana:clap2::clap2::clap2:
 

chonde isiwe balaa, wala sijazwe mawaa,
mkwepe hizo fadhaa, japo mepita wasaa,
enzi mlipozitwaa, siku zile mling'aa,
ingekuwa kitambaa, kila mtu angevaa,

sasa himiza vijana, himeni zao watunze,
waepushe danadana, tabia njema wafunze,
si usiku si mchana, bila ndoa wasianze,
ngekuwa kitambaa, kila mtu angevaa,
 

hehehehe!
NAOMBA NIMSINDIKIZE KOLOKWINI KWA WOMBO....''wana ngonjeera jama twaondoookaa,wana ngonjeeraa jama twaondoookaaaa!upepoooooo bahariiiniiiiiiii MAWIMBI YANA TUPEPERUSSHAAAAA''
 
HONGERA SANA JUDY

nimekupenda ghafla
 
hehehehe!
NAOMBA NIMSINDIKIZE KOLOKWINI KWA WOMBO....''wana ngonjeera jama twaondoookaa,wana ngonjeeraa jama twaondoookaaaa!upepoooooo bahariiiniiiiiiii MAWIMBI YANA TUPEPERUSSHAAAAA''


Msaada Hauna RISITI!
:msela::msela:
 

kukwepa hiyo ni tabu, kwa vile ni maumbile
tangu enzi za mababu, miaka ya enzi zile
twapenda hii dhahabu, ikitajwa pumzi tele
japo hakuna sababu, hupigwa vigelegele
 
hehehehe!
NAOMBA NIMSINDIKIZE KOLOKWINI KWA WOMBO....''wana ngonjeera jama twaondoookaa,wana ngonjeeraa jama twaondoookaaaa!upepoooooo bahariiiniiiiiiii MAWIMBI YANA TUPEPERUSSHAAAAA''
hehehe dah! teamo bana!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…