Deadline yangu mwakani, ndoa lazima nifunge

Tunaoondoka selaaa, tunayumbayumbaaa selaaa
Wanamashairi selaa,
Mimi na Teamo selaaa
Iyooyoo selaaa
..UPEPO WA BAHARI KWA MAJONZ UNATUPULIZA...LY TWAAGA WADOGO ZETU(asprin na rr ndo wadogo zetu)
 
p fankkkkkkkkkk wap??????!!!!!!!!!
ntakupromote.....:first:
 

babu asipirini, maumivu wayatuliza,
tena wajaa hisani, katu huwezi kuliza,
iwayo ile sirini, huko nako waliwaza,
babu nakuamini, kwa yote ulonijuza,

japo wataja talaka, hiyo kwangu hakuna,
heri nivae viraka, hiyo daima takana,
bila kufanya haraka, watu hawataachana,
babu nakuamini, kwa yote ulonijuza

ndoa kwangu sio vita, rahaye kama peponi,
na vita vinaposita, wajeshi cheko usoni,
bali ndoa kisita, chozi tele machoni
babu nakuamini, kwa yote ulonijuza
 

Hahahahahahahahahhahahahahhah

Kumrithi dada Judy, babu anakosa gani?
Eti mlio weledi, swali hili swali gani
Nimeamua nirudi, nielewe kiundani
Maana babu bepari, Judy uwe makini

Atajifanya kukagua, matiti kwa kuanzia
Bila wewe kutambua, kumbe babu avizia
Mwishowe wastukia, bepari keshajilia
Judy babu ukimpatia, na mimi ntanyatia
 
huu utunzi safi sana eeh mungu na mie nipe kipaji cha uzeeni niwe namwimbia wa ubani wangu maishairi yenye vina
 

Hebu tema mate chini, dada Judi nakwambia,
Talaka ziko mfukoni, mwa mumeo nakwambia,
Ukileta kisirani, talaka akutupia,
Omba kwa Mungu mapema, kabla hayajakufika,

talaka kikutupia, angalizo nilikupa
kwa babuyo kimbilia, kawaida sina pupa,
Mikononi takutia, raha zote nitakupa,
Babuyo niko tayari, kukutulizia shida.

Nita kuweka chumbani, udi ntakununulia,
Pafyumu ya arabuni, chumbani takuwekea,
Ntakugandisha moyoni, njia hautapotea,
Babuyo niko tayari, talaka ukipatiwa.
 

haloooo haloooooooooooooo!!!!!!!!....haloooooooo ya babuuuu....kulea WAJUKUUU!!!!!!!!
 

Na wewe Jeneresheni, uzibe waniwekea?
Mwenzio niko kazini, mbona unanibania,
Naitimiza zangu fani, wewe waniharibia?
Undugu undugu gani, Nguguyo wambania?

Wengine mechakachua, shangazi mmewaita,
Kisa kuniharibia, Au mnataka vita?
Wengine nakuachia, Da Judi hutampata,
Undugu undugu gani, Nguguyo wambania?
 


judith best angu,naomba uwe wifi angu
nakukaribisha uje kwetu,uongeze idadi yetu
uwe mama wa wanetu,hilo kwetu tashukuru.
nakuomba judith,uje kabla ya dedilaini.

tumezaliwa watatu,mimi na kaka zangu,
wamenipa kazi tatu,kuwachagulia wa kudumu
asiwe sistaduu,wala wa kupiga vibomu
nakuomba judith,uje kabla ya dedilaini.

sifa za nimpendae,wa kuja kua wifi angu
awe na dini yake,inayomwabudu mungu
asiwe na dunia yake,inayopenda majungu
nakuomba judith,uje kabla ya dedilaini.

kama ubeti wa tano,sifa zake zimo
njoo kwa maringo,hadi kwa mzee timo
tutachinja majogoo,kukukaribisha nditto
nakuomba judith uje kabla ya dedilaini.

kaka zangu mapacha,wote mahendisamu,
wanafanya kazi moja,makazi darisalamu
wakisafiri wiki moja,kurudi haraka muhimu
nakuomba judit uje kabla ya dedilaini

mimi si wifi mtata,nimefunzwa mila zetu
wifi angu tampenda,uwe kama ndugu yetu
mana sina hata dada,wewe takua best angu.
nakuomba judit,uje kabla ya dedilaini.
 

:clap2::clap2:😛opcorn:😛opcorn:
 

Du! mi sijui ntoke vipi? Hongereni washairi wote....................
 

goood birungi!:clap2::clap2::clap2::clap2::first:
 

birungi nakujilia, kicheko mefungulia,
ombilo nafikiria, kakazo wasaidia,
kama tamthilia, akili yanigomea,
mimi bado kuijua, mbeleko ya kubebea

kakazo wako wawili, mie mdada mmoja,
yangu dhaifu misuli, yatosha mume mmoja,
katu sidhani bahili, wote takuwa kioja,
mimi bado kuijua, mbeleko ya kubebea

hakika u mkarimu, kwenu wanikaribisha,
mie sinayo laumu, upendo menionesha,
wahidi hata karamu, wifiyo mkaribisha,
mimi bado kuijua, mbeleko ya kubebea

huo ubeti wa tano, hakika yote yakini,
lau upate maono, hima taleta kidani,
utamaliza vinono, Judi kumleta ndani,
mimi bado kuijua, mbeleko ya kubebea

sasa nakupa shauri, kama mmoja ni radhi,
huyo alete mahari, pia apime maradhi,
nae mwenyewe akiri, kama ataka nihodhi
mimi bado kuijua, mbeleko ya kubebea
 

asante wifi angu,kwa ombi kulikubalia
nilifikisha azma yangu,kuwambia wangu makaka
sikiliza jibu langu,kuhusu hawa mapacha
wote ni kaka zangu,jichagulie doto au kulwa

wanafanana haiba,sura hata na tabia
wote hawana hasira,malezi wanayajua
ni wakarimu na subira,ni wepesi kuelewa
wote ni kaka zangu jichagulie doto au kulwa.

sitaki kupendelea,kukusakizia doto
nani atakua na kulwa,wa kumzalia watoto
najua wahitaji mmoja,umfanye wako mto
wote ni kaka zangu jichagulie kulwa au doto.

we sikiliza moyo wako,nani awe chaguo lako
tutatii ombi lako,mahari tutaleta kwa mikogo
kama ni kulwa au doto,hamna atakaeona kinyongo
wote ni kaka zangu,jichagulie kulwa au doto.

nadhani nimekujibu,wasiwasi nimekuondoa
maradhi kupima muhimu,kuna mengi hii dunia
kua na mmoja udhu,si mapenzi ya kuchangia
wote ni kaka zangu,jichagulie kulwa au doto
 
Dah nipe na mimi masharti ya vina vizani nitoe hoja!
 


babu nna wasiwasi,fani yako ina ukakasi
vipi upo kila nafasi,hata mjukuu wamjia kasi
si kidogo utapigwa pasi,vijana wana mingi mitikasi
wajukuu hatutaki kesi,kuletewa maovu yako na maasi.
 
Miss all the bets.
Mh kwenye vina kati na mwisho cmooooooooo!
Ila kuna beti ya majibu mstarri wa mwisho nahisi umechanganya beti ya tisa badala ya beti ya sits! Nimehisi tu, kama haina makosa bac cjaielewa.
 
Miss all the bets.
Mh kwenye vina kati na mwisho cmooooooooo!
Ila kuna beti ya majibu mstarri wa mwisho nahisi umechanganya beti ya tisa badala ya beti ya sits! Nimehisi tu, kama haina makosa bac cjaielewa.

kuna beti nyingi sana za majibu kwa watu tofauti, labda unisaidie ni post # ngapi ili nikaiedith. thanks
 

Babu nomaaaaaaa.....I rest my case!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…