Deal Done: Harry Maguire atua rasmi Manchester United

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Hatimaye Manchester United na Leicester City wamekubaliana dau la Pauni 80 milioni kwa beki wa kati Harry Maguire.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 anatarajiwa kufanyiwa vipimo pale Manchester United wikiendi hii.
Anakuwa mchezaji wa tatu kusainiwa katika klabu ya Manchester United katika dirisha hili, wengine wakiwa ni Aaron Wan-Bissaka na Daniel James ambao walitua wakitokea Crystal Palace na Swansea kwa mfuatano huo.
Tangu amejiunga na Leicester City akitokea Hull City mwaka 2017, Maguire amecheza mechi 69.
Usajili huo unamaanisha kwamba Maguire amekuwa beki ghali zaidi duniani akipiku kiasi cha Pauni 75 milioni ambacho Liverpool waliilipa Southampton ili kumnasa Virgil van Dijk Januari, 2018.
United walikuwa wakimtafuta Maguire kwa muda mrefu lakini walishindwa kumnasa miezi 12 iliyopita hiyo ni kwa kuwa mchezaji huyo alikuwa na dau kubwa zaidi wakati Man United walikuwa tayari kutoa Pauni 70 milioni.
 
ana jipya gani huyo jamaa zaidi ya goal la faulo worl cup?
 
Badilisha hapo katika ' Headline ' yako Kiingereza sahihi ( cha Mwingereza / Briton ) Mwenyewe mwenye Lugha yake ni DONE DEAL na siyo DEAL DONE tafadhali. Kila la Kheri Mkuu.
 
Lakini kuna utofauti 'Mkubwa' tu wa taarifa kuhusu 'Ada ya Uhamisho'.

Kuna wanaosema "Paundi Milioni 80" huku wengine wakiongeza na kusema "Paundi Milioni 85".

Utofauti wa Paundi Milioni 5 si mdogo!
 
Angalau sasa tupumzike maana nilichoka kila siku kumskia
 
Anazidiwa takwimu na beki mbovu pale Arsenal mustafi
IMG_20190802_234725.jpeg
 
Lakin angesajiliwa kwenye timu yako unayoishabikia ungefungua na Uzi kabisa kumnadi kwa sifa kibao ..maisha hayaendi bila unafiki..anasemaga Edo kumwembe
Man united wangemchukua coulibaly wa napol ndo angewazima watu mdomo yule ndo beki kisiki kwelkwel kaka ila huyo Maguire Hana tofauti kubwa na kina mustafi,Phil jones,Smalling na ungechanganya na Hilo dau yaani hapo man u kapigwa kweupe.
 
Sio mbaya wala mzuri kama mnavyompamba ,

Ukitaka kuamin subir atakavyokuwa anawasindikiza Mawinger kama Pepe ,Salah ,au Rahim
 
Back
Top Bottom