Deal ya Ali Kiba na Sony: Makosa yanayojirudia..

Umesahau kwamba Keko wa Uganda na Redsan wa Kenya walisign mkataba. Tofauti na matararajio yako, nyimbo zao zinauza sana ulaya na marekani kuliko Africa!
Wanamuuzia nani ulaya na marekani??? Kama nyimbo zao zinauza sana kwanini Keko analia na kuwalaani Sony wanamshusha kimziki???
 

Mdakuzi,

Kwanza kabisa unapotosha watu wasiofahamu unapoanza kutoa mifano eti drake ana mkataba na Sony lakini bado ana management yake au AKA wa SA! Mikataba yao iko tofauti kabisa na mkataba wa Ali.. Kuna watu wako Sony ila mkataba yao inahusu distribution tu ya mziki wao (hasa kwenye mitandao).. Mkataba wa Ali kwa mujibu wa wao wenyewe walivyotutangazia ni kwamba utahusu kuanzia production, distribution, marketing na management (labda kama mlizidisha mbwembwe mpaka mkaongea uongo).. Sasa hapo ndipo kwenye wasiwasi wangu! Wasanii wote (Africa) ambao wamesaini mkataba wa dizaini hii wamepotea kwenye mziki, kama ni coincidence basi hii itakuwa ni super coincidence!! Kwanini hawana hata msanii mmoja Africa wanayeweza kujivunia kama mfano????

Na usipotoshe kwa mifano ya kina AKA, mkataba wa Ali uko tofauti kabisa! Kuna mikataba ambayo ukisaini na Sony hata wakizingua inakuwa ngumu kukupoteza! Mfano msanii kama Ryan Leslie ninavyoelewa ni kuwa ana makubaliano na Sony kwa ajili tu ya ku-access studio zao! Yani wana makubaliano Ryan Leslie anaweza kuingia katika studio zao na akafanya production ya nyimbo yake Basi! Lakini masuala mengine yote yanasimamiwa na kampuni zake za Next Selection na Renegades!

Alafu hiyo mifano ya Dee kuwa na mikataba na kampuni za Nigeria iko irrelevant kabisa! Makubaliano ya Dee na hao jamaa ni sawasawa tu kama ilivyo na watu kama Mikito hapa bongo!! Nothing big! Alafu hizo ishu sijui dili aliyounganishiwa na Kikwete haijasainiwa mpaka leo, Duh sasa hiyo inahusika vipi na tunachoongelea hapa??? Au ndo kutaka kutuambia kuwa Jamaa wamekataa kusaini na Dee wanamuona hana kipaji ila Ali kasaini na Sony ndio ana kipaji, hahahaahahh!! That's too low mkuu, argument za kijiweni!! Ni kama kipindi kile Seven anawashawishi MTV wasipige nyimbo za Dee kwa matarajio kuwa Dee akishuka Ali atapanda matokea yake yamekuwa tofauti kabisa!!

Turudi kwenye point, natamani ungetuonyesha record ya Sony katika kumsaidia msanii yeyote wa Afrika kuvuka mbali zaidi!! Umesema Mkataba wa Davido na Ali unafanana, well let's wait and see maana Davido ndio kasaini mkataba na Sony mwezi January tu kama sikosei so hatuwezi kumchukua kama mfano (ingawa nimeanza kuona chenga chenga)..

Namtakia Ali kilala heri na natamani kuona stock yetu ya wasanii wa kimataifa kutoka TZ inaongezeka na nimekuwa nikimuangalia Ali kama msanii potential anayeweza na yeye siku kuwa wa kimataifa lakini nadhani washauri wake wanamuangusha sana, management imejaa wajuaji wasioweza kutumia ujuaji wao na kwenye hii dili mmemuingiza chaka msanii wetu.!!?
 
Kuna ubaya gani nikimpongeza au Nina ugomvi nae gani??? Na kuna ubaya gani nikitoa angalizo ambalo labda linaweza kumsaidia msanii mwingine??? Ubaya unao uona wewe uko wapi???
ukijiongeza utafahamu kuwa rockstar ni moja ya kampuni mama za Sony pia alikiba sio msanii mdogo na hiyo deal ni globally soma kwenye source magazine wameandika hiyo issue kwa upande Wa alikiba mwenye mashabiki wengi east Africa hii itamsaidia sana ukiwa serious
 
Let's wait and see! Ninachotaka ni kwamba achukue tahadhari tu, asijione amelamba dume hao jamaa hawana record nzuri Africa
 
naona povu tu mitandaoni uwiii kiba sio mtu mzuri hata kidogo Kuwa label moja pamoja na Davido, Chris brown, John legend na beyonce sio jambo la kitoto lazima wauza tomato povu liwatoke
 
Its not a 'global deal'! Ila si unajua wabongo kwa kuongeza chumvi

Kiba na Davido ndiyo wasanii pekee wa Africa waliopata global deal, sasa nashangaa jamaa yangu povu linakutoka hahaha
 
Mkuu so point yako (Kama sijakosea) ni kiba na management yake wasikungekubali kusign na Sony music Africa?

Ni kama kushangilia ndoa huku hujui kama itakuja kuwa na matunda!!!
 
Its not a global deal!
Kwanini Sio Global funguka Mkuun tofauti na hapo unaweza onekana mpiga mjungu maana yeye mwenye mkataba anasema ni global wewe unasema sio global.

ukifanya hivyo utasaidia wengi kama mimi.
 
Jinyonge kama imekuuma nyie ndo vikwazo vya maendeleo na kama unajfanya unajua hadithi anzisha thread tuzsome na sio kukalia majungu we mkataba wa kiba unakuhusu nin fuatlia maisha yako
 
Jinyonge kama imekuuma nyie ndo vikwazo vya maendeleo na kama unajfanya unajua hadithi anzisha thread tuzsome na sio kukalia majungu we mkataba wa kiba unakuhusu nin fuatlia maisha yako
Hahahah!! Wewe kama sio mpiga kigodoro basi utakuwa memba wa bendi bati ya misuto kitaa..
 
Its not a global deal! Trust me.. its just a "publicity stunt" kuitangaza hivyo but the deal is not global

Kwaiyo Iyo page Ya Twitter Ya source ni waongo !!!!!? Na kwa nini wewe ufikirie ni uwongo!!!! Publicity ili wapate nini source !!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…