Nadhani haikuwa busara kuwa na haraka ya kuuponda mkataba............
Na kuna mkataba wa pili wa kushiriki kuanzia maandalizi ya product ya msanii hadi kwenye kutafutia masoko.
Alikiba na AKA (Aliyeimba na Nassib) wote wako chini ya Sony Music ila mikataba yao inatofutiana, mkataba wa Alikiba unafanana kila kitu na mkataba wa Davido.
Ni mkataba unaoanzia katika maandalizi ya product ili kuipa thamani zaidi, pia kuwaunganisha wasanii wa label yao kufanya kazi za pamoja (collabo).
Mdakuzi,
Kwanza kabisa unapotosha watu wasiofahamu unapoanza kutoa mifano eti drake ana mkataba na Sony lakini bado ana management yake au AKA wa SA! Mikataba yao iko tofauti kabisa na mkataba wa Ali.. Kuna watu wako Sony ila mkataba yao inahusu distribution tu ya mziki wao (hasa kwenye mitandao).. Mkataba wa Ali kwa mujibu wa wao wenyewe walivyotutangazia ni kwamba utahusu kuanzia production, distribution, marketing na management (labda kama mlizidisha mbwembwe mpaka mkaongea uongo).. Sasa hapo ndipo kwenye wasiwasi wangu! Wasanii wote (Africa) ambao wamesaini mkataba wa dizaini hii wamepotea kwenye mziki, kama ni coincidence basi hii itakuwa ni super coincidence!! Kwanini hawana hata msanii mmoja Africa wanayeweza kujivunia kama mfano????
Na usipotoshe kwa mifano ya kina AKA, mkataba wa Ali uko tofauti kabisa! Kuna mikataba ambayo ukisaini na Sony hata wakizingua inakuwa ngumu kukupoteza! Mfano msanii kama Ryan Leslie ninavyoelewa ni kuwa ana makubaliano na Sony kwa ajili tu ya ku-access studio zao! Yani wana makubaliano Ryan Leslie anaweza kuingia katika studio zao na akafanya production ya nyimbo yake Basi! Lakini masuala mengine yote yanasimamiwa na kampuni zake za Next Selection na Renegades!
Alafu hiyo mifano ya Dee kuwa na mikataba na kampuni za Nigeria iko irrelevant kabisa! Makubaliano ya Dee na hao jamaa ni sawasawa tu kama ilivyo na watu kama Mikito hapa bongo!! Nothing big! Alafu hizo ishu sijui dili aliyounganishiwa na Kikwete haijasainiwa mpaka leo, Duh sasa hiyo inahusika vipi na tunachoongelea hapa??? Au ndo kutaka kutuambia kuwa Jamaa wamekataa kusaini na Dee wanamuona hana kipaji ila Ali kasaini na Sony ndio ana kipaji, hahahaahahh!! That's too low mkuu, argument za kijiweni!! Ni kama kipindi kile Seven anawashawishi MTV wasipige nyimbo za Dee kwa matarajio kuwa Dee akishuka Ali atapanda matokea yake yamekuwa tofauti kabisa!!
Turudi kwenye point, natamani ungetuonyesha record ya Sony katika kumsaidia msanii yeyote wa Afrika kuvuka mbali zaidi!! Umesema Mkataba wa Davido na Ali unafanana, well let's wait and see maana Davido ndio kasaini mkataba na Sony mwezi January tu kama sikosei so hatuwezi kumchukua kama mfano (ingawa nimeanza kuona chenga chenga)..
Namtakia Ali kilala heri na natamani kuona stock yetu ya wasanii wa kimataifa kutoka TZ inaongezeka na nimekuwa nikimuangalia Ali kama msanii potential anayeweza na yeye siku kuwa wa kimataifa lakini nadhani washauri wake wanamuangusha sana, management imejaa wajuaji wasioweza kutumia ujuaji wao na kwenye hii dili mmemuingiza chaka msanii wetu.!!?