Dear mama....


Pole yako ni amali,kwani yatoka moyoni,
nitailinda ka mali,hujatoa kimatani,
imetulia ka asali,mwangu ikae moyoni,
Nakushukru mkuu,pamoja daima tupo,
 

Sina la kuongezea,yote umeyatimiza,
kila mtu analegea,kusikia zako miza,
nami ndo nazipokea,moyoni kuzitimiza,
Wewe ni wangu kaka,ndugu wa fani na vina,
 


Magulumangu huishi nikosha , kwa yako matamu maneno
Mimi leo tena wanikosha, kwa yako kwa mama maneno
mama nami huitwa , mamayo wamuita kwa yako maneno
mimi kama mama nahakiki, mama kapokea yako maneno

Samahani Magu naishia, shairi darasa bado napewa
Lizzy mwalimu nasifia, kwa uvumilivu wote napewa….



Will be cont...
 
Lizzy kwa maishair azid kunikosha
Ninachoweza kukushauri...

Aaah mi nimeshindwa bana lizzy hahaha
Uda'a umenichekesha..kama huwezi ulikuwa unajaribu ya nini
 
Duniani we ndo MUNGU wangu mama/
jinsi navyokupenda moyoni hutanihama/
chozi lako linapotoka moyo unanichoma/
tangu a,e,i,o,u vidudu niliposoma/
hadi chuo kikuu maujanja nasoma/

huwa nanumia unapokuwa mbali/
ninapokumiss nalia kama sina akili/
kitu gani nikupe cha kifahari/
hela,nyumba,au gari la kifahari/
naomba usinitenge hii maisha kamari/
 


Na nyie ndugu zanguni, mnaniliza jamani,
Ninaumia moyoni, hili pigo maishani,
Jamani sana poleni, yatoka kwangu moyoni,
Mametu hawa wawili, walale pema peponi.

Walale pema peponi, Semeni wote amina,
Waimbe sana mbinguni, itikieni amina,
Wakae nayo amani, Semeni tena amina.
Wote tena kwa sauti, tuitikie amina
 

Mdau Yakuonea, Salamu nakutumia,
Kofia nakuvulia, ushairi waujua,
Vina unavipangia, kadhalika mizania,
Hakika wewe malenga, malenga ulotukuka.

Hakika wewe malenga, malenga ukotukuka,
Mashairi wayapanga, yametulia hakika,
Hakuna atayepinga, unazi sijauweka,
Hakika wewe malenga, malenga ulotukuka.
 

Asha D salamu,

Hauvumi lakini umo..... kaza buti mama!...........Nakufagilia!
 
Pole sana ndg, kilichobaki ni wewe sasa kujiandaa kiroho ili uwe safi muda wote. Kweli mama is the best how ever she is! Heshima kwa wamama woooote popote pale walipo including myself:dance::dance::dance:
 
NDUGU YANGU ASPRIN

Asante nakushukuru, malenga ulokomaa
Watupa tungo za nuru, na mengi yenye kufaa
Liongoze hili duru, wewe kweli kifaa
salamu nazipokea, ndugu yangu asprin

Ningali ni mwanafunzi, ushairi sijajua
Natamani niwe mjuzi, lugha kudadavua
Mola naomba nienzi, nichanue kama ua
Salamu nazipokea, ndugu yangu asprin

Asprin u mkongwe, hilo wote twatambua
Hufanyi yenye mizengwe, na fani unaijua
Tuongoze kwenye ngwe, fani ipate kukuwa
Salamu nazipokea, ndugu yangu asprin

Na pale kwenye makosa, naomba nisahihishe
Tafadhali anza sasa, nisije patwa kasheshe
Tupende yetu sanaa, ujumbe tuufikishe
salamu nazipokea, ndugu yangu asprin

Hapa ninaweka nanga, wewe uwangu mwalimu
Nitakuja hata Tanga, nipate yako elimu
Mola sikupe majanga, maisha yako yadumu
salamu nazipokea, ndugu yangu asprin


 
What is more important she found joy being who she was..........................nobody forced her into womanhood.......she knew a calling was hers alone when it came knocking at her door...........................................................
 

Dua zako twashukuru, amina twaitikia
Hata awe zeru zeru , Mama ndio dunia
Mama tukimkufuru, maisha tayachukia
Utazimaliza duru, dhalili utaishia
 
Kloro nimesikia, mama nguzo ya dunia
Utakuja jijutia, mama sipomsikia
Laana akikuachia, Maisha yatafifia
Mama zetu ni dunia, hata awe zeruzeru

Mama akikasirika, hima omba msamaha
Kweli utaabika, mama akikosa raha
Mwilini utadhurika, ubaki na majeraha
Mama zetu ni dunia, hata awe zeruzeru

Mama akifurahika, twapata nyingi thwawabu
Maisha yatanyooka, tazama kwenye vitabu
Na katu hutopotoka, usiwe ni mwenye tabu
Mama zetu ni dunia, hata awe zeruzeru

Mama zetu tuwaenzi, kwa mema yao malezi
Hawa kwetu ni wajenzi, tuwape nyingi pongezi
Tusifanye ya ushenzi, mama pokea mapenzi
Mama zetu ni dunia, hata awe zeruzeru


Dua zako twashukuru, amina twaitikia
Hata awe zeru zeru , Mama ndio dunia
Mama tukimkufuru, maisha tayachukia
Utazimaliza duru, dhalili utaishia
 

Ubarikiwe yakuonea, kwa mema maneno
Wengi tumekusikia, umenena kwa mifano
Uwazi umetuwekea,wala hukuuma meno
Mama ndie malkia , ameshinda mashindano

Sina la kuongezea, yote umeyamaliza
Atakae puuzia , dunia itamfunza
Ewe ulo maridhia, haya maneno sikiza
Alotupa yakuonea, yakutoe kwenye giza
 
Kila nikifikiria, machozi yanizidia
Hebu Kloro fikiria, mangapi walipitia
Shida ziliwazidia, bado walivumilia
Mama zetu mama zetu, bado ningali nalia

Roho taweka rehani, mamangu asidhurike
Napenda yake amani, mabaya yasimfike
Nasema kweli jamani, bora hai mnizike
mama zetu mama zetu, ningali bado nalia

Nashindwa hata andika, sijui niseme nini
Mama yangu kwa hakika, mfano wake sioni
Nitazusha patashika, mama kipatwa huzuni
Mama zetu mama zetu, ningali bado nalia

 
Mkuu kloro yaani nimejikuta suddenly nime-fall in love na mashairi sikuwahi kuandika mashairi maishani mwangu lakini niliamini naweza na nilipojaribu kuandika nimejikuta niko in love
 

Nasaha naziongeza, kwa walo ndani ya ndoa
Wenza wasijetuponza, mama tukamshushua
Mama yeye ni kwanza, wengine wanafatia
Sitochoka kuhimiza , mama namfagilia

Hisia zisikubebe , ndugu yangu yakuonea
Kula tena ushibe, uikabili dunia
Kwenye pengo tulizibe, Mama atakusifia
Uiname kama kobe, anapotunga sheria

Jihadi yahitajika , mama kumtetea
Bunduki nimejitwika, ya shairi sikia
Nawatafuta mateka, mama walomsusia
Tuwapige mweleka, njia kuwanyooshea.

Ni jukumu letu sote, JF na dunia
Slaa hata Kikwete, umuhimu waujua
Tusimameni kidete, mama kumhudumia
Tutabarikiwa wote , na muumba wa dunia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…