So the talent was hiding inside u, sasa naomba ujiamini kwasababu uko juu vibaya sana kwenye hii fani hata nimeanza kukuogopa. Pia am glad kusikia kwamba nimekuwa part ya inspiration kwako.
Naona mwanisifia, tungo mwazifurahia
Mwasema ziko sawia, na tena mmeridhia
Vina mwaniambia, hakika vinatishia
Nawashukuru wenzangu, ningali najifunzia
Kutunga nilitamani, toka zama za zamani
Labda sikujiamini, ningeanzaje jamani
Leo nipo furahani, najaribu hii fani
Nawashukuru wenzangu, ningali najifunzia
Ni kweli sijakomaa, ningali ni mwanafunzi
sitokata na tamaa, nipate mwingi ujuzi
Mola nipe shufaa, ili niwe mkufunzi
Nawashukuru wenzangu, ningali najifunzia
Msaada mnipatie, enyi mliobobea
Msiniache nikimbie, bahari kuogelea
Kweli mnisaidie, tungo zisije pelea
Nawashukuru wenzangu, ningali najifunzia