"Mwanakijiji, mimi sikufahamu, lakini nimelazimika kukuandikia ujumbe huu mfupi, maelezo uliyoyaeleza kwenye barua kwenye gazeti la mwana halisi, ulichoeleza ni muhimu watu wajue kuwa ukoloni mambo leo umepitwa na wakati, vitisho vimepitwa na wakati, wakoloni walichokiacha ndicho kinachoendelea mpaka leo.
Maana yake mtanzania hatakuwa huru mpaka pale atakapofunguliwa macho aone, wakati huyu mheshimiwa aitwae kipenzi cha watanzania, kikwete, alisema maisha bora kwa kila mtanzania, lakini hatufichi hakuna kilichofanyika, watanzania wana hali mbaya kuliko kawaida, wamenyanga'nywa mali zao nyumba zao, baada ya kukopeshwa na taasisi za fedha, pride, finca, na zingine za aina hiyo.
Ikainuka Deci, iliyotusaidia sana walala hoi, na sasa unasikia ilivyoendelea kuambiwa ni upatu, sasa mwisho wa mambo haya hatujajua nini kitatokea, ila waambie wazi c.c.m. Mwisho wake ndio huo, imetudanganya inatosha, sasa wananchi wanasema liwalo na liwe, hatuwezi kukubali
kupoteza fedha zetu kijinga, wakati serkali yetu ilitoa leseni, sawa hawakufanya ilivyotakiwa, walikuwa wapi?
Tukisema kuwa serkali ya c.c.m. Imetuibia ni sawa. Nalosema mwakani haiwezi kurudi madarakani. Tumeamua, wanachana lak 7. Na wale walionyuma yetu jumla ni m.3. Kama c.c.m. Inataka mioyo yetu irejee watupe hela zetu, kinyume chake. C.c.m. Kwa heri, haitarudi madarakani tena.
Jambo jipya laja. Waambie, waandikie, wameshindwa kuwabana mafisadi walioiba mabilioni, leo wananyang'anya walala hoi vimtaji vyao walivyowekeza Deci. Ok. Inzi kufia kwenye kidonda ni halali yake, jambo laja, hatutanyamaza, nasema jambo laja. Laja. Laja. Asante, sipendi jina langu litajwe, ila mambo ndio hayo. Damu yamwagika nchini. Oh."
Nyie wajinga hamumtishi mtu.
Ndomaana ujinga wa kupindukia hauishi nchi hii. Mijitu kwa tamaa ya pesa na uvivu inajiingiza kwenye upatu afu ikiliwa inaanza kulia na serikali.
Nasema hapana. Wacha wajinga waliwe ili wajifunze. Na mkawasimulie watoto na wajukuu wenu ili wasirudie huu ujinga nao wakaliwa.
The government cannot protect you from your own recklessness.
Na lolote liwe. Do your worst.
There is no such thing as a free lunch. Habari ndo hiyo. Ebo!