NgomaNzito
JF-Expert Member
- Jan 10, 2008
- 559
- 28
Kuna tetesi kuwa ile Kampuni ya DECI (T) ltd imenyimwa kibali na Central Bank (BOT) cha kuanzisha Scheme nyingine inayoitwa Elimika Scheme inayohitaji mwanachama kutoa Sh milion tano upate sh. Milion 12.5 ndani ya wiki 22.
Tetesi hizi zinadai pia Deci inaweza kuingizwa kwenye adminstration na central bank very soon baada ya kuonekana mabosi wake wanafuja fedha za wanachama kwenye scheme yao ya TRF ambapo mwanachama anapaswa atoe kati ya sh laki mbili apate laki tano. Kwa mwenye taarifa zaidi amwage hapa tuwajadili kwa watz wengi wamewekeza kwenye huu mfuko......
Kibali wlichonacho DECI ni kwa mwanachama kupanda si zaidi ya Sh laki mbili kwa mwanachama lakini wao wanawashurutisha wanachama wapande zaidi ya fedha hiyo na hapo ndio kilio kitakapotokea kwa wanachama wadanganyikaMbona sijaifahamu scheme hii inaonekana ni poa kwa wajasiliamali kama ipo sustainable. Lakini sijaelewa unato milion 5 unapata milion 12 ndani ya 22 weeks. Wao wanawekeza wapi kuweza kuzalisha pesa ya kumlipa mteja pesa zote hizo. Inaonyesha wanakulipa riba 30% kwa mwezi, hata treasury bills hazina interest yaaina hiyo. Wanapaswa kuchunguzwa ili kujua machanics ya biashara yao.
Kuna tetesi kuwa ile Kampuni ya DECI (T) ltd imenyimwa kibali na Central Bank (BOT) cha kuanzisha Scheme nyingine inayoitwa Elimika Scheme inayohitaji mwanachama kutoa Sh milion tano upate sh. Milion 12.5 ndani ya wiki 22.
Tetesi hizi zinadai pia Deci inaweza kuingizwa kwenye adminstration na central bank very soon baada ya kuonekana mabosi wake wanafuja fedha za wanachama kwenye scheme yao ya TRF ambapo mwanachama anapaswa atoe kati ya sh laki mbili apate laki tano. Kwa mwenye taarifa zaidi amwage hapa tuwajadili kwa watz wengi wamewekeza kwenye huu mfuko......
Sasa Ngabu hapa tukueleweje? kuwa huyu dada kaibiwa na DECI anawaza fweza zake zilivyokwenda au hebu tufafanulie
Naona bado kidogo watu waanze kulia. Nakumbuka ile hadithi ya nyani na wanunuzi wa nyani! Sasa wameshaanza kuadimika sasa